STEVE NYERERE AKUBALI YAISHE, AUKACHA UTEUZI SHIRIKISHO LA MUZIKI,AJIUZULU NAFASI YA USEMAJI

 STEVE NYERERE AKUBALI YAISHE, AUKACHA UTEUZI SHIRIKISHO LA MUZIKI,AJIUZULU NAFASI YA USEMAJI



Msanii wa Filamu nchini Steven Mengele, maarufu kama Steve Nyerere leo ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi ya usemaji wa shirikisho la muziki hapa nchini.

Steve ambaye uteuzi wake uliwagawa wanachama wa shirikisho hilo katika makundi mawili ya  wanaomtaka na wasiomtaka amesema ameamua kuchukua uamuzi huo ili shirikisho hilo lisiparaganyike na badala yake wawe kitu kimoja.

Aidha ameongeza kuwa hana uhasama na msanii wa hip hop hapa nchini Hamis Mwinjuma maarufu kama MWANA FA na wao ni marafiki na itaendelea kuwa hivyo.

Uteuzi wa steve Nyerere kama msemaji wa shirikisho la muziki mapema wiki iliyopita ulileta sintofahamu kubwa kwa wadau wa sanaa hapa nchini jambo lililogawanya katika makundi wasanii wakimshutumu aondoke katika nafasi hiyo kwa kigezo cha kutotambua uteuzi wake licha ya baraza lililomteua kukiri kuwa walifuata taratibu katika uteuzi wake.

Comments