Watanzania waonyesha kumchagua Rais Samia kwa asilimia 75.
Watanzania waonyesha kumchagua Rais Samia kwa asilimia 75.
Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Refine Data Tech yenye makao makuu yake nchini Estonia umeeleza kwamba ikitokea Uchaguzi Mkuu ukafanyika kipindi hiki Rais Samia Suluhu Hassan angeshinda kwa asilimian 75.
Akiwasilisha maoni hayo ya Watanzania leo Jijini Dar es Salaa,
katika mkutano na waandishi wa Habari Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo
Sonja Ohra-aho amesema utendaji wa Serikali ya Awamu ya Sita Watanzania
wameonyesha kuuami na kukubaliana na juhudi za Rais Samia kwa kipindi
chake cha mwaka mmoja cha kuiongoza Tanzania.
Aidha amesema kuwa katika matokeo ya utafiti huo jumla ya
Watanzania 8,960 walishiriki katika kutoa maoni haya ambapo wanawake ni
asilimia 56 na wanaume asilimia 44 na usajili wa wapiga kura ni asilimia
87.
Ametaja sababu ya Rais Samia kuchaguliwa kwa asilimia 75 kuwa ni
kutokana na kuendeleza miradi ya kimkakati ambapo ameeleza kuwa asilimia
67 ya washiriki wamesema Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi ya
kimkakati kwa zaidi ya asilimia 61.
“ Sababu nyingine za Rais Samia kukubaliwa na Watanzania ni
mapambano yake dhidi ya rushwa ambapo tunaona asilimia 55 ya washiriki
wamesema Serikali imejizatiti kupambana na rushwa kwa zaidi ya asilimia
41″Amesema Sonja Ohra-aho, Na kuongeza kuwa
“Kitu kingine ni kusimamia haki, usawa, amani na utangamano,
ambapo tunaona kwamba asilimia 39 ya washiriki wamesema Serikali imeweza
kulinda haki na kudumisha amani, usawa na utangamano kwa zaidi ya
asilimia 91”
Hata hivyo amesema vita dhidi ya Uviko-19 zimefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutokana na maoni ya Watanzania kuonyesha kuwa asilimia 70 ya
washiriki wamesema Serikali imefanikiwa kupambana na Uviko-19 kwa zaidi
ya asilimia 61.
Katika upande wa uongozi wa Rais Samia, amesema maoni ya
Watanzania yameonyesha kwamba asilimia 76 wanasema ni mzuri, asilimia 14
mbaya na asilimia 10 wastani.
Sambamba na hayo amesema jambo ambalo Watanzania wanavutiwa
katika uongozi wa Rais Samia ni vita dhidi ya Uviko-19 asilimia 25,
kujenga uchumi asilimia 11, ushirikiano na vyama vingine asilimia 14,
utoaji ajira asilimia 4, kusikiliza wananchi asilimia 10 na kuendeleza
miradi ya kimkakati asilimia 36.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa mihimili ya Serikali, maoni ya
Watanzania yameonyesha kuwa asilimia 88 ya Watanzania wamesema Rais
Samia amefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.
Katika suala la ujenzi wa uchumi kwa mujibu wa maoni hayo
asilimia 60 ya washiriki wamesema Serikali imeweza kujenga uchumi kwa
zaidi ya asilimia 61 ambapo katika upande wa ushirikiano wa kimataifa,
kutokana na kujenga mahusiano ya kimataifa asilimia 80 ya washiriki
wamesema Serikali imeweza kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa zaidi ya
asilimia 61.
Comments