CUF YATANGAZA MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA CHAMA,YAMTEUA HAMAD MASOUD HAMAD KUWA KATIBU MKUU.
Dar es salaa,Tanzania
Mwenyekiti wa Chama
cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema baraza kuu la chama hicho
limemteua Ndugu Hamad Masoud Hamad kuwa katibu mkuu wa chama hicho.
Profesa Lipumba
ameyasema hayo mara baada ya kuzungumza na wanahabari ofisi ya makao makuu ya
chama hicho,Buguruni Jijini Dae es salaam alipokuwa akizungumzia maazimio
mbalimbali ya kikao cha baraza kuu la uongozi la chama hicho lililokutana march
24 na 25 jijini humo.
Aidha mwenyekiti huyo
amewapongeza wanachama wa chama hicho waliorejea katika chama mara baada ya
kuondoka katika vyama walivyohamia kwa
kile walichodai haki inapatikana ndani ya chama hicho na kuongeza kwa
kipindi hiki wamewaruhusu wanachama hao kugombea nafasi za uongozi ndani ya
chama katika uchaguzi utakaofanyika may 14 mwaka huu katika jumuiya zote za
chama hicho.
Katika hatua nyingine
ameiomba serikali kuangalia namna ya kupambana na tatizo la mfumuko wa bei
kwani linawaumiza wananchi wengi na kuwasababishia maisha magumu huku akitoa
wito kwa Urusi na Ukraine ambao ni wazalishaji wakubwa wa ngano na mafuta ya
alizeti kuketi meza moja ili kuzungumnza na kufikia muafaka wa kusitisha
mapigano yanayoondoa mamia ya wananchi wasio na hatia na kuongeza kuwa chama
hicho hakipendezwi na hatua ya Urusi kuivamia na kuishambulia nchi ya Ukraine.
Kuhusu suala la
katiba mpya na tume huru ya uchaguzi Prof Lipumba amesema suala hilo ni muhimu
na chama chake hakijapendezwa na maoni ya kikosi kazi kiluichodai suala hilo
lishughulikiwe mwaka 2025 baada ya uchaguzi.
Comments