ACT WAZALENDO CHAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA KWA WATOROSHAJI MADINI,CHASHAURI KUANZISHWA KWA BENKI YA MADINI.

ACT WAZALENDO CHAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA KWA WATOROSHAJI MADINI,CHASHAURI KUANZISHWA KWA BENKI YA MADINI.

Na mwandishi wetu,

Dar es salaam

Chama cha Act Wazalendo kimetoa wito kwa serikali kupitia wizara ya madini kuendelea kuzuia mianya ya utoroshwaji wa madini kwa kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya bajeti ya Wizara ya Madini kusomwa Bungeni Jijini Dodoma Msemaji wa kisekta, Sekta ya Madini ya chama hicho Edgar Mkosamali amesema ni wakati wa serikali kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ya madini na kanuni zake.

Aidha amesema  kutokana na Serikali kushindwa kutekeleza matakwa ya sheria ya madini inayoitaka serikali kumiliki  asilimia 16 ya hisa katika makampuni  madini kumechangia katika kupekekea upotevu wa mapato kwa serikali kutoka sekta ya madini.

Hata hivyo ameitaka serikali kuanza kutenga fedha katika bajeti yake walau asilimia tano kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo Tanzania ambao huchangia asilimia 30 ya pato la taifa kupitia sekta ya madini.

“Asilimia 30 ya mapato ya sekta ya madini yanatokana na wachimbaji wadogo ila hadi sasa serikali bado haiwajali ili hali sera inasema serikali itawezesha ili kukua kwa kuwaelimisha na kuwapatia mtaji na vifaa hivyo ni vyema serikali ikaanzisha benki ya madini ili isimamie mikopo na  wachimbaji wadogo wa madini kwani ni vigumu kwa benki za kawaida kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo”  Amesema Mkosamali. 

Sambamba na hayo ameshauri serikali kuziwezesha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi kwa kuendana na ukuaji wa sekta hiyo kwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia inayotumika duniani





Comments