BISHOP ROSE MGETTA AWEKWA WAKFU KUWA ASKOFU MKUU,MAKANISA YA MLIMA WA MOTO TANZANIA

 BISHOP ROSE MGETTA AWEKWA WAKFU KUWA ASKOFU MKUU,MAKANISA YA MLIMA WA MOTO TANZANIA



Askofu wa kanisa la mlima wa moto TAG Mikocheni B Rose Joseph  Mgetta leo amewekwa rasmi wakfu wa kuwa Askofu mkuu wa makanisa ya Mountain of fire Tanzania 'mlima wa moto' hapa nchini.

Sherehe za kuwekwa wakfu kwao  Askofu huyo zinafanyika hii leo katika kanisa la mlima wa moto Mikocheni JIjini it Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makanisa na serikali.

Askofu Rose Mgetta alisimikwa rasmi kuwa Mchungaji kiongozi wa kanisa la mlima wa moto Mikocheni miezi michache baada ya kifo cha aliyekuwa Askofu mkuu wa makanisa ya mlima wa moto marehemu Bishop Mama, Getrude Rwakatare ambapo leo Askofu Mgetta amewekwa wakfu kuwa Askofu mkuu wa makanisa ya mlima wa moto Tanzania

Askofu Rose Joseph Mgetta ni mzaliwa wa Tanga na mke wa jaji Joseph Mgetta na mama wa watoto watano ambaye alitumika katika kanisa hilo kwa miaka mingi na baadaye kama Mchungaji kiongozi wa makanisa ya mlima wa moto,msomi mwenye diploma na degree katika theolojia ya mambo ya uongozi na utawala na leo amekuwa rasmi Askofu mkuu wa makanisa hayo.

Mchakato wa kumpata kiongozi huyo mkuu wa makanisa ya mlima wa moto ulianza baada ya mwasisi wa kanisa hatari Dr GETRUDE Rwakatare kufariki DUNIA na baadaye kanisa kubaki chini ya usimamizi wa kamati  kuu iliyosimamiwa na watoto wake pamoja na viongozi wakuu na baadaye kumchagua Askofu Rose Mgetta kuwa kiongozi mkuu wa makanisa ya mlima wa moto Tanzania na baadaye kupitia vikao vya kamati kuu ilipendekezwa asimikwe kwao mujibu wa katiba 


Comments