Skip to main content

ILI KUEPUKANA NA UKAME,JAMII YASHAURIWA KUONGEZA JITIHADA MADHUBUTI.

 

ILI KUEPUKANA NA UKAME,JAMII YASHAURIWA KUONGEZA JITIHADA MADHUBUTI.
Mkurugenzi Msaidizi huduma za ramani kutoka Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Elizabeth Mrema akizungumza na waandishi wa habari  Aprili 25,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi kutoka RCMRD Keneth Kasera akizungumza na waandishi wa habari  Aprili 25,2022 Jijini Dar es Salaam.

****

Mkurugenzi Msaidizi huduma za ramani Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Elizabeth Mrema ameitaka jamii kuongeza jitihada za makusudi kuhakikisha wanayatunza mazingira yaliyowazunguka ikiwemo vyanzo vya Maji ili kusaidia kuepukana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea ikiwemo hali ya ukame.

Rai hiyo ameitoa leo Jijini Dar es salaam katika Warsha iliyohusisha watalaam wa Mazingira kutoka Nchi wanachama wa RCMRD ambao wamekutana kwa siku mbili kwa ajili ya kujadili mradi unaotumia teknolojia ya ramani kwa ajili ya kuangalia uharibifu wa vyanzo vya Maji.

Hata hivyo Elizabeth amesema kwamba mradi huo ni wakutumia satelaiti kupata taarifa za uchafuzi wa Mazingira ambapo umeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2016 chini ya Shirika la Msaada la Marekani( USAID ),nakwamba umeonekana kuwa na manufaa makubwa kwa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika katika kubaini vyanzo vya uharibifu wa Mazingira .

"Tunashirikiana na kituo Cha RCMRD kilichopo nchini Kenya kwani Tanzania ni miongoni mwa Nchi ishirini wanachama wa kituo hiki tangu mwaka 1975 ambapo kituo hiki kinatoa mafunzo yaliyojikita kwenye rasilimali ardhi ikiwemo Maji,ardhi ,milima pamoja na Misitu" amesema Elizabeth.

Kupitia Warsha hiyo ya siku mbili itasaidia kubaini changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa mradi huo wa majaribio na kutoa ushauri kwa viongozi wa serikali za Nchi wanachama wanaohusika katika utunzaji wa rasilimali za kwenye ardhi ikiwemo vyanzo vya asili hususani vyanzo vya Maji.

Kwa upande wake Keneth Kasera kutoka RCMRD amesema kwamba lengo na madhumini yakufanyia warsha hiyo hapa nchini nikuonyesha kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa kituo hicho waliobahatika kupata mradi wa majaribio utakaokua na manufaa makubwa kwa wananchi wake.

"Ramani na picha tulizofanyia utafiti wa mradi huu wa majaribio uliodumu kwa miaka sita sasa tutazionyesha nakuzijadili kwa pamoja ili tutoke na maadhimio ya pamoja yakwenda kuzishauri Serikali zetu nini kifanyike ili masuala mbalimbali ya ardhi ikiwemo vyanzo vya Maji viweze kutunzwa" amesisitiza Keneth

Nae Calvin's Wara kutoka RCMRD upande wa Masuala ya Adhi amesema kwamba tayari wameshafanya majaribio katika Mto rufiji,Ziwa Chald na maeneo mengine nakubaini changamoto zinazopelekea uharibifu wa rasilimali zilizopo kwenye ardhi na kusaidia kupata ufumbuzi wakr

Aidha jamii inatakiwa kutambua kuwa utunzaji wa raslimali zilizopo katika ardhi ni muhimu sana kwani inasaidia mwanadamu kuishi katika Dunia pasipokuwa na majanga yeyote ya asili.

Comments