MAKALLA AIPONGEZA MACHINGA COMPLEX KWA KUANDAA SIKU YAO MAALUM,AWAAHIDI USHIRIKIANO THABITI

 MAKALLA AIPONGEZA MACHINGA COMPLEX KWA KUANDAA SIKU YAO MAALUM.



Na Thadei PrayGod
Dar es salaam

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos MAKALLA ameupongeza uongozi wa soko la machinga complex liliopo ILALA Jijini humo kwa Kuandaa maonyesho maalum ya wajasiriamali wa soko hilo yenye lengo la kukuza biashara sambamba na Kuandaa siku maalum ya machinga complex ambayo imeadhimishwa leo na kutanguliwa na maonyesho makubwa ya biashara,pamoja na michezo mbalimbali


RC Makala ametoa pongezi hizo leo Aprili 25,2022 wakati akizindua rasmi maonyesho ya siku ya machinga complex ambapo amesema jambo hilo limeendelea kulipa heshima kubwa soko hilo.

 RC MAKALLA pia amewataka wanaopotosha umma kuwa soko hilo halina wafanyabiashara waache tabia hiyo kwani soko hilo lina wafanyabiashara lukuki wakiwemo wale waliotoka soko la kariakoo.

"kuna watu wanapita pita huko mitaani na mitandaoni mara ooh soko la machinga complex halina wafanyabiashara sasa hawa mnaowaona hapa wamejaa ni akina nani?nawaomba waache kupotosha kuhusu soko hili kwani ni soko lenye kila aina ya bidhaa"alisema RC Makalla

Pia ameahidi kuendelea kuwa balozi mzuri wa kulitangaza soko hilo lenye kila aina ya biashara huku akiwahakikishia kuendelea kulilinda soko hilo kwa kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara hao.

"Rais wetu wa serikali ya awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan ameboresha miundombinu ya masoko mbalimbali hapa Dar es salaam ikiwemo hili la machinga complex hivyo sisi kama wasaidizi wake tutaendelea kutoa ushirikiano kwa nyie wafanyabiashara  ili kuhakikisha Taifa linaendelea kukua kiuchumi.

Kwa kujibu wa meneja wa soko la machinga complex Stella Mgumia,Siku ya machinga complex pia imeenda sambamba na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa pete pamoja na michezo mingine inayohusisha timu za wafanyabiashara hao ambayo itazidi kujenga mahusiano mema miongoni mwao wafanyabiashara na kuwajenga kiafya.


Comments