WAZIRI MKUU AZIPA MAAGIZO WIZARA UENDELEZAJI KIJIJI CHA MSOMERA, HANDENI

 WAZIRI MKUU AZIPA MAAGIZO WIZARA UENDELEZAJI KIJIJI CHA MSOMERA, HANDENI




*********************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa maeitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha shughuli za ujenzi katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Makoani Tanga zinakamilika haraka.

 


Amesema kuwa Wizara hiyo inapaswa kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari. "Zoezi hili linaloendea la kuimarisha miondombinu ikiwemo upimaji wa viwanja litawanufaisha wakazi wa Msomera pamoja na hao wanaohamia eneo hili.”


 

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumapili, Aprili 24, 2022) alipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Mkoani Tanga kwa ajili ya wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhamia kwenye Kijiji hicho ili kupisha shughuli za uhifadhi kwa maendeleo ya Taifa.


Aidha, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kuandaa mazingira mazuri ya ufugaji. “Wizara hii inapaswa pia kuhakikisha kwamba kunakuwa na miundombinu wezeshi ya wafugaji yakiwemo malambo ya kunyweshea mifugo, majosho, ujenzi wa kliniki ya kutibu magonjwa ya mifugo katika eneo hilo.”


 


Akitoa maelekezo kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka iendelee kuwekeza nguvu katika kuimarisha miundombinu ya elimu. “Kama tunavyoona hapa shule ya msingi inajengwa, sekondari inajengwa, zahanati zinakarabatiwa lakini pia ujenzi wa kituo cha afya na barabara unaendelea, ongezeni nguvu.”


 


Mheshimiwa Majaliwa pia ameitaka Wizara ya Maji iendelee kuhakikisha kiwango cha maji katika eneo hilo kinakuwa toshelevu kwa kuchimba zaidi ili hata majosho na malambo yapate maji ya kutosha. Maji ambayo tayari yameshachimbwa na kuyapata ni mengi kuliko mahitaji lakini tuongeze kiwango.”


 


Pia, Waziri Mkuu alisema kuwa Watumishi wote wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliojenga katika hifadhi ya Ngorongoro hawataingia kwenye utaratibu wa kupewa nyumba kwa kuwa walivunja sheria. “Nataka niwaambie watumishi wa NCAA mliojenga kule, tutaondoa nyumba zenu zote kwasababu mmevunja sheria, kama unajua umejenga anza kuondoka mwenyewe

Comments