Skip to main content

ACT WAZALENDO YAWEKA WAZI MAPENDEKEZO YAKE WALIYOPELEKA KWA KIKOSI KAZI CHA RAIS SAMIA,YATAKA RUZUKU IWE KWA VYAMA VYOTE

 ACT WAZALENDO YAWEKA WAZI MAPENDEKEZO YAKE WALIYOPELEKA KWA KIKOSI KAZI CHA RAIS SAMIA,WATAKA RUZUKU KWA VYAMA VYOTE.

Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ismail Jussa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama cha ACT-Wazalendo Dorothy Semu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ado Shaibu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam.


Na mwandishi wetu,Dar es salaam

Makamo mwenyekiti wa chama cha ACT WAZALENDO,Dorothy Semu amesema ACT imewasilisha kwa kikosi kazi Maoni yake juu ya masuala mbalimbali ikiwemo la ushiriki wa wanawake na watu wenye makundi maalum katika  masuala ya kisiasa.


Bi Semu ameyasema hayo wakati akiyasoma maoni yaliyopelekwa katika kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia ambapo,
Ameongeza kuwa makundi hayo yamekuwa nyuma kushiriki katika shughuli za kisiasa ikiwemo kudhihakiwa na kutukanwa katika majukwaa hayo pindi wapatapo nafasi hizo hivyo wameshauri kamati hiyo kuwa kuwe na orodha ya viongozi hasa ngazi za bunge kupeleka majina ya wagombea yanayozingatia usawa wa kijinsia na kuzingatia wenye ulemavu ili kuwe na uwiano mzuri kisiasa kwa makundi hayo.

Amesema mfumo huo utaondoa dhana ya kupanga juu ya nani atashiriki na kushinda uchaguzi katika jimbo husika na utakuwa wa haki kutokana na kuwa na uwazi na suala la elimu ya uraia liondolewe katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na liwe ni jukumu la vyama hivyo katika kutoa elimu hiyo kwani bado kuna watanzania ambao hawajapata elimu ya uraia ipasavyo jambo linalosababisha wengi wao wasijue umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi.

Aidha kuhusu suala la rushwa katika uchaguzi  amesema kuwa chama hicho kinaamini kuwa suala hilo liendelee kufanywa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa,na kuifanya takukuru kama msimamizi mkuu wa kushughulikia masuala ya rushwa katika chaguzi mbalimbali sambamba na kuboreshwa kwa sheria ya vyombo vya habari ili vitekeleze wajibu wao kwa huru na haki wa kutobagua vyama vya kuripoti habari zake.

Naye karibu mkuu wa chama hicho,Ado Shaibu amesema kufuatia kikao cha kamati kuu visiwani Pemba 22/06,2022 na baadaye 23/05,2022 maoni ya kamati hiyo yakapelekwa mbele ya kikosi kazi kilichoundwa na   Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yakihusisha hoja mbalimbali.
Kusudio la chama hicho ni kupeleka maoni hayo pia kwa umma kupitia vyombo vya Habari na baadaye kwa wanachama wake nchi nzima.

Pia amesema moja ya maoni yaliyopelekwa kwa kikosi kazi hicho cha Rais ni pamoja na kufutwa kwa kifungu cha sheria namba 11(2) kinachotaka mamlaka matumizi ya vifungu vya 43-46 vya sheria ya jeshi la polisi katika mchakato wa uitishwaji wa mikutano ya siasa kubwa ni lazima chama kiombe ruhusa hiyo kwa jeshi la polisi ili kipate kibali na badala yake jeshi hilo libaki kama msimamizi tu wa masuala ya ulinzi na kiusalama katika mikutano hiyo na si kuingilia kwa kuizuia.

Suala la Ruzuku kwa vyama vya siasa chama hicho kimetoa maoni kuwa ni lazima vyama vyote vyenye vigezo vya kupata Ruzuku,vipewe ruzuku ili kuviwezesha katika kujiendeleza kuachana na utaratibu wa sasa ambao ni vyama vyenye madiwani na wabunge pekee ndiyo vinaweza kupata ruzuku na kuwepo kwa mchanganuo wa ni kiasi gani kila chama kinastahili kupata.

"na pia tumeona ni lazima vyama vinavyopata Ruzuku viwe ni vile ambavyo havitakuwa na hati chafu kutoka ofisi ya mkaguzi wa hesabu na zaidi ya asilimia 30 ya viongozi wake wawe ni wanawake ili vyama vingi zaidi vya siasa vilivyo makini vipate Ruzuku"aliongeza Ado Shaibu.

Aidha kwa upande wake mjumbe wa kamati kuu ya Act WAZALENDO,Ismail Jusa amesema kuwa pia chama hicho kimetoa maoni yake kuhusu suala la katiba ambapo amesema katiba iliyopo hivi sasa iliandaliwa enzi za ukoloni na baadaye kufanyiwa mabadiliko machache  katika utawala wa hayati Mwalimu Nyerere ambapo pia ilikuwa ni kama maoni ya mtu mmoja na kufanyiwa tena marekebisho na kisha kutungwa katiba ya mwaka 1977 ambayo inatumika mpaka hivi sasa na kama chama kinaona maoni ya wananchi wengi hawakushirikishwa katika katiba hiyo hivyo watanzania wanahitaji kuwepo kwa katiba mpya.

"Kwa kuwa utaratibu wa katiba pendekezwa hatukufanikiwa hadi baadaye kupatikana kwa katiba hiyo ambayo pia inaonekana haina sifa ya kuwa katiba mpya kwani iliyapiga teke maoni mengi ya wananchi na kam msimamo wa chama tunahitaji katiba mpya na mchakato wake unapaswa kuanza sasa na tunahitaji kuwepo kwanza kwa mwafaka wa kitaifa tukutane pamoja na kujadili juu ya muundo wa katiba mpya utakaoshirikisha makundi yote katika jamii''alisema Jusa.

Pia amesema Act WAZALENDO imeshauri kuwa ni lazima kuwepo kwa mapitio ya sheria ya tume ya mabadiko ya katiba na ile ya maoni ya rasimu ya  katiba hiyo ili kuuboresha mchakato huo wa kupatikana kwa katiba mpya.

Kuhusu suala la uchaguzi ameendelea kuwa ni lazima kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo ndiyo itakuwa msimamizi wa kupatikana kwa katiba mpya.

Na tume hiyo ipewe kazi pia ya kuajiri watumishi wake wote ambao wataridhiwa na vyama vyote vya siasa nchini.

Comments