JUKWAA LA WALIMU WAZALENDO TANZANIA LAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA JITIHADA ZAKE KULETA MAENDELEO
JUKWAA LA WALIMU WAZALENDO TANZANIA LAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA JITIHADA ZAKE KULETA MAENDELEO


Na Thadei PrayGod
Dar es salaam.
Jukwaa la walimu wazalendo Tanzania limeipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo mbalimbali ambayo yameleta mafanikio makubwa hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Katibu mkuu wa jukwaa hilo Anuary Ally Mgonde amesema kuwa mafanikio aliyoyaleta Rais Samia kwa kipindi kifupi cha uongozi wake ni cha kusifika ulimwenguni.
Ameongeza kwa kitendo cha Rais Samia kuongeza mishahara kwa asilimia 23.3 tena katika kipindi hiki chenye changamoto lukuki za kiuchumi hivyo kama Tanzania inatakiwa kuendelea kumtia moyo Rais Samia.
“ndugu wanahabari tumeona mama yetu Samia amefanya makubwa ikiwemo zaidi ya walimu 25,000 ambao wameajiriwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wake na amejenga madarasa zaidi ya 15,000 ambayo kwa mara ya kwanza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari kuingia shuleni kwa awamu moja jambo ambalo limewasaidia walimu kufundisha kwa kwenda sambamba na mitaala sisi kama walimu tunaishukuru sana serikali”alisema Anuary.
Aidha amesema kitendo cha Rais Samia kuongeza kiasi cha mikopo inayopaswa kukopeshwa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu pamoja na kuondoa asilimia 10 ambazo walikuwa wanatozwa wahitimu waliochelewesha kulipa mikopo yao ni jambo jema na limeongeza idadi ya wanafunzi ambao wataendelea na masomo yao ya elimu ya juu na hivyo kutengeneza Taifa lenye vijana wengi wenye elimu.
Ameongeza kuwa Kuna baadhi ya watu wanamsema vibaya Rais Samia ambaye amehamishwa wananchi wanapata maji safi na salama,elimu bora,miundombinu bora,huduma bora za afya hivyo tusiwe watu wa kumtukana na kumdhihaki kwani anafanya kazi kubwa na wao kama jukwaa la walimu wazalendo wako pamoja naye.
Kuhusu filamu ya Royal Tour Jukwaa hilo limesema kuwa limekusudia kutengeneza mabalozi wa Royal Tour Film mashuleni kwa kuwaeleza maana na faida za filamu hiyo kwani wengi wa wanafunzi hawatumii mitandao hivyo elimu hiyo itajenga kizazi bora kwani walimu ndiyo msingi wa kutengeneza Taifa na pia watahakikisha wanafunzi wanatembelea vivutio vya utalii.
hapa nchini kujionea mazuri yake na kuongeza kuwa watafanya makongamano nchi nzima kuanzia ngazi ya chini ili kuelimisha jamii hasa ya chini juu ya kuisemea filamu hiyo.
Hata hivyo katika hatua nyingine jukwaa hilo limewataka watanzania kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi agosti mwaka huu ili kuusaidia serikali kutambua idadi ya watu hali itakayosaidia katika kupanga mipango yake ya maendeleo katika kuliendeleza Taifa na watu wake.
Jukwaa hilo pia limezindua kauli mbiu ambayo wataitumia katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Samia inayosema “NASIMAMA NA MAMA”


Comments