KAMATI YA AFYA BUNGE LA ZAMBIA YATEMBELEA KIWANDA CHA KAIRUKI PHARMACEUTICAL LTD TANZANIA
KAMATI YA AFYA BUNGE LA ZAMBIA YATEMBELEA KIWANDA CHA KAIRUKI PHARMACEUTICAL LTD TANZANIA
Meneja wa kiwanda cha madawa cha Kairuki Pharmaceutical LTD kilichopo Kibaha mkoani Pwani Ellen Magita akizungumza na wanahabari akieleza kuhusiana na ujio wa Kamati ya Afya ya Bunge la Zambia ambao wametembelea Kiwanda hicho leo kwa ajili ya kujifunza.Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na jamii ya Bunge la Zambia Dkt Christopher Kalila akizungumza na wanahabari akieleza dhumuni lao la kutembelea kiwanda cha madawa cha Kairuki Pharmaceutical LTD. Baadhi ya mitambo ya kuzalisha Chupa za maji tiba katika kiwanda cha madawa cha Kairuki Pharmaceutical LTD
..................................
Na Mwandishi wetu,Kibaha
Kamati ya Afya ya Bunge la Zambia wametembelea kiwanda Cha Kairuki Pharmaceutical LTD Nchini Tanzania ili kujifunza namna ya kuwekeza katika viwanda vya dawa vya wazawa bila kutegemea wafadhili kutoka nje ya Nchi.
Ziara hiyo wameifanya leo kwenye kiwanda hicho kinachopatika na Kibaha Mkoani Pwani ambapo imeelezwa kina uwezo wa kuzalisha Chupa za maji tiba Mill.55 kwa Mwaka na mpaka sasa tayari wamepeleka zaidi ya chupa Mill 1 katika bohari ya Dawa.
Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa kiwanda cha madawa cha Kairuki Ellen Magita amesema kuwa ujio wa wabunge hao unaweza kuwanufaisha kwa kuweza kupeleka dawa nchini mwao kwa sababu kiwanda kina uwezo mkubwa wa kuzalisha chupa za kutosha.
"Kiwanda hiki kimesimwikwa kwa Teknolojia ya hali ya Juu ambayo Kwa Nchi zote za Afrika Mashariki na kati sisi ndo tunaongoza wa kwanza lakini pia inakubalika na Shirika la Afya Duniani hivyo bidhaa tunazo zitoa zinakubalika kote"amesema Magita
Kuhusu uwekezaji wa Kiwanda hicho Magita amesema ni Shilingi za Kitanzania Bill 47 ndio zimetumika hivyo ameeleza malengo yao ni kuendelea kuisaidia Tanzania na nje.
Aidha ameeleza mitakati ya kiwanda hicho kuwa wanatarajia kuzalisha maji tiba katika ujazo mdogo na ndani ya Miezi 18 watapanua zaidi kuanzia ujazo wa Mills 2 mpaka 20 na wanamaoni ya miaka miwili ya kutaka kuzalisha vifaa tiba vinavyotumika hospitalini
Meneja huyo amezungumzia changamoto ambazo wamekumbana na zo kuwa wameathiriwa na COVID-19 kwani kiwanda hicho kilitakiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2019 lakini kutokana na sababu hiyo kimeanza mwaka 2022.
Kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na jamii ya Bunge la Zambia Dkt Christopher Kalila amesema takriban wabunge 10 wamefika na kutembelea kiwanda hicho yote ikiwa ni kuendelea ushirikiano wa mataifa lakini pia kujifunza namna Tanzania inahusika na utengenezaji wa madawa.
Comments