KATIBU MKUU,NCCR MAGEUZI,ASEMA CHAMA HICHO KI MIKONONI MWAKE,AMPA TUHUMA NZITO JAMES MBATIA

 

KATIBU MKUU NCCR MAGEUZI ASEMA CHAMA HICHO KI MIKONONI MWAKE,AMTUHUMU MAKUBWA JAMES MBATIA.

Katibu mkuu wa chama cha Nccr Mageuzi,Martha Chiomba ameelezea sakata la yeye kutaka kuondolewa ndani ya chama hicho kama jambo linalompa hofu juu ya maisha yake.


 Kupitia mkutano wake na wanahabari hii leo jijini Dar es salaam Katibu mkuu huyo amesimulia kwamba,

Aliitwa nyumbani kwa mbatia na akaombwa awape simu yake ya mkononi na baadaye akaambiwa kuwa kuna vijana ambao wanataka ajiuzulu nafasi yake kama Katibu mkuu na wamashaandika barua na kuisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.


Anasema kuwa baadaye alitakiwa kujiuzulu nafasi hiyo ili kuepusha purukushani ndani ya chama kwa kutakiwa kuandika barua ya kujiuzulu kwake nyadhifa ya Katibu mkuu licha ya wakati huo kuwa mgonjwa hivyo akawaomba wamwandikie barua ya kumtaka kujiuzulu jambo ambalo walikubaliana na kisha kuondoka ndani ya nyumba hiyo.


Anadai kuwa baadaye aliwasiliana na viongozi wengine wa chama hicho kupitia simu ya mtoto wake kwani ilimbidi kubadilisha namba ya simu kwani awali aliambiwa aliwasiliane na mtu yoyote

.

Ameongeza kuwa baada ya kuwasiliana na viongozi wengine akiwemo Anthon Komu walimshauri asijiuzulu nafasi hiyo na badala yake utumike utaratibu kama katiba ya chama inavyotaka jambo ambalo mwenyekiti wake hakupendezwa nalo kwani kuna moja ya wanasiasa waliohamia katika chama hicho kutoka chama kingine ambaye alitaka nafasi yake ya ukatibu mkuu.


Anaongeza kuwa kwenye group moja la chama vijana wa chama hicho walimtukana matusi ya nguoni bila mwenyekiti wa chama hicho kusema lolote licha ya yeye pia kuwamo katika group hilo la WhatsApp wakimtaka ajiuzulu bila hata kuzingatia hali yake ya kiafya,hali iliyopelekea hata maumivu yake kutopata nafuu na mshono aliyoshonwa hospitalini kufumuka nusu.


“Maisha yaliyoko hatarini ni ya mimi Katibu mkuu na siyo kama anavyodai mwenyekiti kuwa yeye yuko hatarini na yeye ndiye anayeongoza genge hilo kwani hata kwenye mitandao mmeoana kuna picha inamuonyesha Edward Simbeye ameshika jiwe kutaka kukishambulia”alisema Katibu mkuu huyo na kuongeza kuwa mwenyekiti wa chama hicho amemfanya ashindwe hata kulala nyumbani kwake kwa kuhofia usalama wake kama mwanamke.

Kuhusu kufukuzwa kwa Mbatia Katibu mkuu huyo amesema kuwa hawajamfukuza ndani ya chama bali kilichobaki ni yeye kufika mbele ya mkutano mkuu utakaoitishwa hivi karibuni na kujieleza.


Kuhusu suala la kwenda kuripoti polisi juu ya kuwa na shaka na usalama wake amesema kuwa tayari ametoa taarifa na ameshakata Rb kituo cha polisi juu ya suala hilo.


Aidha amesema kwa sasa chama kiko mikononi mwake kama Katibu mkuu na amesema atamwandikiia barua James Mbatia kurejesha funguo za ofisi na kama hatofanya hivyo taratibu nyingine zitafuatwa na kuwataka wanawake wa chama hicho na mashirika mengine ya halina wanawake kujitokeza mahakamani endapo atapeleka kesi mahakamani.

Comments