SERIKALI YALIPONGEZA SHIRIKA LA USAID KUPITIA MRADI WA FEED THE FUTURE

 

SERIKALI YALIPONGEZA SHIRIKA LA USAID KUPITIA MRADI WA FEED THE FUTURE


Na Thadei PrayGod,


Dar es salaam.


Serikali kupitia wizara ya kilimo imeipongeza shirika la msaada la kimarekani USAID kupitia mradi wa Feed The Future kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika  kuwaendeleza vijana kupitia kilimo.


Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na naibu waziri wa kilimo,Anthon Mavunde wakati wa hafla ya uzinduaji wa kitabu cha “Feed The Future Tanzania  chenye kuelezea shuhuda za vijana mbalimbali waliofanikiwa kupitia mradi huo wa kilimo na biashara,sambamba ukabidhianaji wa magari mawili yatakayosaidia katika shughuli za kilimo.


Mavunde amesema vijana wengi wamefaidika kupitia shirika hilo kupitia programe wanazoendesha kwa kuwafanya wakulima wadogo kuwa wakubwa,na kukuza biashara zao na kuongeza kubwa hiyo ni dhamira njema.


Aidha amesema kama wizara wataendelea kuliunga mkono shirika hilo na kuongeza kuwa magari waliyokabidhiwa yatatumika katika miradi wa kuwaendeleza vijana kwenye kilimo na wataanza katika mkoa wa Dodoma Mwezi Julai ambapo kuna wakati zaidi ya elfu ishirini.


Amelipongeza shirika hilo pia kwa kumpatia magari hayo mawili aina ya LandCruiser Hardtop yatayosaidia katika shughuli za kilimo.


Naye mkurugenzi wa mradi wa feed the future Tanzania,Ngasuma Kanyeka amesema mradi huo uliogadhiliwa na UsAid umekuwa na mafanikio makubwa sana na umewapa vijana nguvu kwa kuwaongezea vijana zaidi ya vijana elfu 42 ambayo ni idadi kubwa kuliko waliyokuwa wakitarajia kufikia ya vijana elfu 33.


Aidha ameongeza kwa lengo la kuzindua kitabu  ni kutaka vijana waonyeshe kwa uhalisia  mafanikio yao kupitia kilimo kwani wengi wamejenga viwanda,nyumba za kuishi na mabadiliko yamekuwa makubwa sana katika maisha yao.

Comments