TALGWU YAKANUSHA MADAI YA UPIGWAJI, FEDHA KATIKA ZABUNI YA KUTENGENEZA SARE ZA MEI MOSI, YASEMA ITALISHTAKI GAZETI LILILOWACHAFUA.

 

TALGWU YAKANUSHA MADAI YA UPIGWAJI, FEDHA KATIKA ZABUNI YA KUTENGENEZA SARE ZA MEI MOSI, YASEMA ITALISHTAKI GAZETI LILILOWACHAFUA.


Katibu Mkuu wa TALGWU,Rashid Mtima Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)Jijini Dar es salaam.


Na Mwandishi wetu,

Dar es salaam.

Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Nchini(TALGWU) kimekanusha habari zinazodaiwa kuwa za upotoshaji zilizotolewa na gazeti la Jamhuri kwa madai ya kupigwa kwa fedha za chama hicho kwenye zabuni ya kutengeneza sare za Mei mosi 2022 pamoja na utata wa manunuzi ya gari la chama hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Mtima amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Jamhuri la tarehe 10 -16  mwezi huu toleo namba 554 lililosomeka kuwa “Fedha za TALGWU zapigwa”ni  taarifa za upotoshaji  kwa umma na wanachama wao ili kuvuruga mshikamano uliopo nakuleta chuki kati ya wanachama na uongozi.


Kuhusu uchapishaji wa sare za Mei mosi 2022 ,Katibu Mkuu huyo amesema kwamba mchakato wa manunuzi ya sare za Mei mosi mwaka huu ulizingatia taratibu zote za manunuzi nakumpata mzabuni ambaye ni kampuni ya Savana General Merchandise ambaye alipewa kazi ya uchapaji na usambazaji wa sare elfu themanini(80,000) zenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 1.1 lakini baada ya mapokezi ya sare hizo zikagundulika kuwa na mapungufu ya ubora ndipo ofisi ilipochukua maamuzi ya kumjulisha mzabuni huyo na kumtaka asimamishe zoezi la usambazaji.


Ameongeza kuwa baada ya kumjulisha mzabuni huyo kuhusu mapungufu hayo pia iliwajulisha makatibu wa chama hicho katika mikoa mbalimbali ambao walikwishapokea sare hizo kutozigawa kutokana na mapungufu ya kiuborat yaliyoonekana katika sare hizo


Katibu Mkuu wa TALGWU Bw.Rashid Mtima amendelea kusema kwamba mzabuni huyo amelipwa kiasi Cha shilingi milioni mia saba(700) pekee Kwa mujibu wa mkataba na siyo bioni 1.1 kama ilivyoripotiwa na Gazeti la Jamhuri.


Kuhusu unuzuzi wa gari Bw.Mtima amewambia waandishi wa habari kwamba katika Gazeti la Jamhuri la tarehe 24 mwaka huu toleo namba 556 lililosomeka kuwa “Utata ununuzi Magari TALGWU” taarifa hiyo ni mwendelezo wa kukichafua na kuzua taharuki Kwa wanachama wake bila sababu za msingi.


” Madai ya gezeti hilo kwamba fedha za ununuzi wa gari ya Katibu Mkuu zilitosha kununua gari jipya lakini likanunuliwa la mtumba, hivyo napenda ieleweke kwamba mchakato wa ununuzi wa gari hili ulizingatia taratibu zote za kanuni za manunuzi ya chama toleo la mwaka 2018 na TALGWU haikuwahi kudhamilia kununua gari jipya kwa kuwa uwezo wa kutenga milioni mia nne( 400) Kwa ajili ya kununua gari la katibu mkuu hatuna”amesema Mtima.

Hata hivyo amesema kwamba bado wanachama wa TALGWU wanaimani kubwa na uongozi wake kwani wanaziona juhudi za uongozi wa chama katika kutetea haki na maslahi yao wakiwa kazini hivyo chama kimejipanga kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Gazeti la Jamhuri kuendelea kutoa taarifa zenye lengo la kukichafua chama na kukidhalilisha.

Comments