TANZANIA, CANADA KUWEKA MKAZO AGENDA YA KIZAZI CHENYE USAWA

 TANZANIA, CANADA KUWEKA MKAZO AGENDA YA KIZAZI CHENYE USAWA

 



Tanzania na Canada zimejipanga kuhakikisha zinachochea maendeleo na ustawi kwa kujikita katika kutekeleza malengo ya jukwaa la kizazi chenye usawa katika eneo la pili la uwezeshaji haki za kiuchumi kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kushughulikia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 


Hayo yamebainika leo Mei 26, 2022 jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima na Katibu wa Bunge la Canada Mhe. Robert Orifant.


Akizungumza katika kikao hicho Waziri Dkt. Gwajima alisema, Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kutekeleza Agenda hiyo na Rais Samia amekuwa kinara katika utekelezaji wake.


Aidha Viongozi hao wamejadiliana kuhusu mpango wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Canada hususan katika masuala ya maendeleo ya Jinsia na uwezeshaji wa Wanawake.


Kwa upande Katibu wa Bunge la Canada Mhe. Robert Orifant alisema, wanafurahia kuona Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kupiga hatua kwenye maendeleo yenye usawa wa kijinsia hivyo, Canada iko tayari kushirikiana na Tanzania kufanya kazi pamoja kwenye maeneo yanayolenga kwenye maendeleo ya wanawake.


Comments