VIONGOZI WA DINI MWANZA WAKOSWHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA,WATOA NENO

  VIONGOZI WA DINI MWANZA WAKOSWHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA,WATOA NENO.

Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa Mwanza ambayo inayoundwa na Viongozi wa Dini mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukutana na kutoa tamko la kumpongeza Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake.
***
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kamati ya Amani ya viongozi wa dini mbalimbali Mkoa wa Mwanza imetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake mzuri katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili tangu aingie madarakani.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Askofu Charles Sekelwa amesema viongozi wa hao wa dini wameamua kujitokeza na kumpongeza Rais Said kwa sababu moja ya jukumu lao ni kukemea, kushauri, kutia moyo na kushukuru pale kwa mambo yote mazuri yanapofanyika.

"Tumekutana kwa ajili ya kumtia moyo, kumpongeza na kumshukuru Rais wetu (Samia Suluhu Hassani) kwa kazi nzuri anazozifanya katika Taifa letu na tunaaamini pongezi zetu ni njia bora ya kumfanya azidi kuwa na hamasa ya kufanya kazi yake vizuri" amesema Askofu Sekelwa.

Aidha Askofu Sekelwa ameleza kuwa uongozi wa Rais Samia umekuwa rafiki katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uhuru wa vyombo vya habari, watumishi kupandishiwa mishahara jambo ambalo linachochea utendaji kazi wenye tija katika Taifa.

Naye Shekh Hassan Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo amesema Rais Samia ameweza kusimamia amani na utulivu wa nchi hali ambayo imesaidia watanzania kuendelea kufanya kazi katika mazingira salama na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.

"Tunamshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa namna ambavyo anazidi kuilinda tunu ya amani tuliyopewa na Mwenyezi Mungu, tunazidi kumuombea ili azidi kufanya kazi zake akiwa na hofu ya Mungu" amesema Sheikh Kabeke.

Kwa upande wake Mchungaji Jacob Mutashi ambaye ni Mshauri wa Kamati hiyo ameeleza kuridhishwa na uongozi wa Rais Samia kwani amekuwa kiongozi wa kipekee anayekutana na makundi mbalimbali katika jamii yakiwemo ya wazee, viongozi wa dini, wanawake, vijana na wafanyabiashara na kutatua changamoto zao huku akiboresha mahusiano baina ya mataifa mengine hatua inayosaidia uchumi wa nchi kuzidi kuimarika.


Credit Binagiblog

Comments