ACT WAZALENDO YATOA MAPENDEKEZO 9, MAKADIRIO YA BAJETI YA NISHATI
ACT WAZALENDO YATOA MAPENDEKEZO 9, MAKADIRIO YA BAJETI YA NISHATI
Dar es Salaam
Chama Cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali isiishie kuweka hutuba ya mkakati wa kutumia nishati mbadala badala yake iwekeze kwenye nishati ya jua, umeme wa maji, gesi asilia Ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yana athari kubwa kwenye mazingira.
Rai hiyo imetolewa na Msemaji wa Sekta ya Nishati ,ACT Wazalendo Is-haka Mchinjita wakati akitoa uchambuzi kuhusu mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2022)23 ambapo amesema bajeti ya mwaka huu ni sh trill 2.91 inaoneka ni kubwa lakini kiuhalisia ni ndogo sana ikilinganishwa na utekelezaji wa Miradi.
"Ukiitaza bajeti ya mwaka huu ni sh trill 2.91 lakini uhalisia wa gharama za miradi katika Sekta ya Nishati ni dhahiri kwamba bado ni ndogo sana, pia ni vyema Serikali ikatoa pesa zilizotengwa kwa wakati Ili kuepusha kulipa gharama za ziada kwa wakandaradi na watoa huduma wengine"amesema Mchinjita.
Aidha, amesema kuwa katika uchambuzi uliofanywa na Act Wazalendo umelenga katika maeneo 9 ikiwemo ufinyu wa bajeti na ucheleweshwaji wa utekekezaji wa Miradi, Utendaji mbovu wa Shirika la umeme Tanesco na kupelekea kuligharimu taifa.
Maeneo mengine ni pamoja na usiri wa mikataba na ukosefu a umakini katika mikataba na kulisababishia Taifa hasara,miradi Mikubwa ya Nishati kutekelezwa kwa kiasi kidogo na kupuuza maslahi ya wananchi katika maeneo ya miradi,kupanda kwa bei ya mafuta, hali ya upatikanaji wa umeme nchini pamoja na gharama za kuunganishiwa umeme,kasi ndogo ya matumizi ya Nishati mbadala na kushindwa kuunganisha umeme katika miradi ya kimkakati ya taifa.
Akizungumzia kuhusu bei za mafuta amesema kuwa, bei za rejareja za mafuta ya Petrol 2,249, Disel 2073na Mafuta ya taa1957 kwa mwezi Julai mwaka 2021 ambapo kupanda kwa bei hizo za mwezi Julai kwa sehemu kubwa zilichangiwa na Sera za Kodi na sheria ya fedha ya mwaka 2021/22 ambayo ilifanya mabadiliko kwa ongezeko la tozo ya mafuta ya sh 100.
"Bei mpya zilizotangazwa juzi na kuanza kutumika June 1, ambazo zimeonyesha kuwa bei ya Petrol sh 2994, Disel 3,131 na Mafuta ya Taa sh 3,299 kuna ongezeko la mwaka mzima sh 745"amesema Mchinjita.
Kwa upande wa hali ya upatikanaji wa umeme amesema bado sio uhakika kumekua na changamoto ya muda mrefu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, kutokana na hali hiyo inabainisha kutosimamiwa vyema vyama upatikanaji wa huduma hiyo.
Aidha amesema wanasisitiza kuwa ni muhimu kwa Serikali kufungamanisha Sekta za uzalishaji na Sekta ya Nishati Ili kuokoa gharama tunazotumia kwenye uzalishaji ambazo hazilinufaishi taifa la Tanzania.



Comments