Na Thadei PrayGod
Dar es salaaam
Kama wewe ni miongoni mwa watazamaji na wafuatiliaji wazuri wa vipindi mbalimbali kupitia dikoda za Azam Tv basi bila shaka utakuwa umekutana na tangazo la spidi 160 sio UTANI',ambalo lilikuacha na maswali mengi kichwani bila kupata jibu sahihi.
Sasa taarifa ikufikie kuwa hii leo kampuni ya Azam TV LTD kupitia, Azam TV wametangaza kushusha rasmi bei ya KISIMBUZI (dikoda) yake ya dish kutoka Tsh 210,000 hadi shilingi 160,000 ambayo itaanza rasmi kuanzia kesho nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya posta, Kijitonyama Jijini Dar es salaam leo June 30,2022 wakati wa hafla ya kutangaza punguzo hilo,Afisa mwendeshaji mkuu wa kampuni ya Azam TV Ltd Loth Mziray amesema lengo la kuzindua kampeni hiyo ya Azam TV si UTANI' na kupunguzwa Kwa bei ya Kisimbuzi hicho Cha dish ni ili kutoa maudhui bora Kwa watazamaji wake na kufikisha lengo lao la kuwafikia watanzania wote, ndani na nje ya nchi.
"Kama mnavyojua ndugu waandishi wa habari Azam TV hatupo tu Tanzania pekee Bali tumefika hadi Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na hivi karibuni tumeingia Zimbabwe na tumeifikia dunia nzima kupitia Azam Max, ndiyo maana tunasema hatuchagui, hatubagui, anayetutazama au kutusikiliza hatumjui na haya yote ni kuendeleza burudani bila kuleta utani hapa Tanzania na ndo maana tunasema Azam TV, burudani Kwa wote" alisisitiza Bwana Loth Mziray
Ameongeza kuwa Azam TV wamekuwa na Nia madhubuti kuwafikia wananchi wote na ndiyo maana wameweka maudhui bora Kwa watu wa rika zote na kuwataka watanzania waifuatilie Azam TV hasa katika chaneli ya Sinema Zetu ambayo itakuwa ya kusisimua zaidi kwan kuendelea kuonyesha filamu na tamthilia bora za kitanzania.
Kuhusu maudhui ya kimichezo Mkuu wa kitengo Cha michezo Azam TV Bi Christina Koroso amesema licha ya kuwa na kipindi cha mapumziko mafupi mara baada ya kumalizika Kwa ligi kuu ya Tanzania bara NBC bado kutakuwa na vipindi bora vya michezo kupitia Chanel za Azam TV HD ikiwemo Kilonga Cup, michuano ya mpira wa kikapu ya Dar es salaam Basketball league, TFF Under 20 pamoja na kipindi kipya Cha Viwanjani ambacho kitaangazia michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Comments