FILAMU YA ‘VUTA NIKUVUTE’KUFUNGUA TAMASHA LA ZIFF, ZANZIBAR.
FILAMU YA ‘VUTA NIKUVUTE’KUFUNGUA TAMASHA LA ZIFF, ZANZIBAR.
![]() |
| Mkurugenzi wa tamasha la ZIFF,Prof Martin Mhando Akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)Jijini Dar es salaam juu ya maandalizi ya tamasha hilo la filamu la nchi za Jahazi. |


![]() |
| Baadhi ya wageni na waandishi wa habari wakifuatilia Kwa makini maelezo juu ya tamasha la kimataifa la filamu la nchi za jahazi,ZIFF ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia June 18,2020 ngome kongwe,visiwani Zanzibar. |
Na Thadei PrayGod,Dar es salaam.
Filamu ya kitanzania ‘Vuta,nikuvute’inatarajia kuwa filamu itakayofungua tamasha la kimataifa la filamu la nchi za jahazi (ZIFF)linalotarajia kufanyika kuanzia June 18,2022,visiwani Zanzibar
Kwa mujibu wa waandaaji na waratibu wa tamasha hilo Kubwa la filamu wanasema filamu ya vuta,nikuvute ni Moja kati ya filamu bora kabisa hapa nchini na Afrika ya Mashariki Kwa ujumla na ndo maana imefanywa kama filamu itakayofungua tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 25 mwaka huu tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mtendaji wa ZIFF,Prof Martin Mhando amesema tamasha hilo kwa mwaka huu litashirikisha filamu zaidi ya 101 kutoka nchi zaidi ya 33 duniani.
Amesema filamu hizo ambazo zitaonyeshwa wakati wa tamasha hilo ni pamoja na filamu kutoka,Afrika ulaya na baadhi ya filamu kutoka America na linatarajiwa kuhudhuriwa na wageni kutoka nchi mbalimbali duniani.
Aidha aliongeza kuwa,Pia siku ya tarehe 19 filamu ya African Redemption itaonyeshwa ambayo itafuatiwa na filamu za Afrika ya kusini kesho yake ikieleza mchango wa Taifa hilo katika kuleta maendeleo katika bara la Afrika,kupitia mtu mweusi.
Ndugu wanahabari tulipokea filamu nyingi sana lakini chache ndizi zilizokidhi vigezo na zitaonyeshwa katika tamasha la ZIFF,Zitafuatiwa filamu mbambali kutoka mataifa ya ulaya na Marekani sambamba na kuendeshwa kwa warsha mbalimbali za kuwaandaa watayarishaji wa filamu juu ya utayarishaji wa miswada ya filamu.
Hata hivyo amesema Mwaka jana walipata zaidi ya watanzania 50 ambao walijitokeza kupata mafunzo hayo na wanatarajia kupata watanzania wengi kwa mwaka huu.
Akizungumzia tamasha hili Balozi wa Nchi za Ulaya, Bwana Manfredo Fanti alisema kuwa, ZIFF ni kiungo muhimu kati ya tamaduni za dunia kupitia uoneshaji wa filamu.
"Filamu ni sehemu muhimu ya kuwasiliana kimataifa, kuelimisha jamii na ajira, hasa kwa vijana. Tunashirikiana na ZIFF kupanua wigo wa taaluma ya filamu hapa nchini kupitia mafunzo na maonesho kama haya,” aliongezea




Comments