HAKI ELIMU YAPONGEZA ELIMU BILA MALIPO KIDATO CHA 5 NA 6,YASHAURI NYONGEZA YA RUZUKU MASHULENI.
HAKI ELIMU YAPONGEZA ELIMU BILA MALIPO KIDATO CHA 5 NA 6,YASHAURI NYONGEZA YA RUZUKU MASHULENI.

Dar es salaam.
Shirika la Haki Elimu limeipongeza hatua ya serikali ya kuongeza Bajeti katika sekta ya elimu hapa nchini.
Taarifa ya shirika hilo lisilo la kiserikali imepongeza hatua ya kupotia bajeti hiyo kugusia maeneo mbalimbali muhimu katika sekta ya elimu ambayo kama yatafanyiwa kazi kama ilivyokisudiwa,ni wazi kuwa yatachangia maboresho katika utoaju na upatikanaji wa elimu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi mtendaji wa haki elimu Dkt John Kalage amesema Bajeti ya sekta ya elimu ambayo ni trilioni 5.6 ambayo ilisomwa bungeni na Waziri wa fedha Kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni ongezeko kutoka trillion 5.3 Kwa bajeti iliyopita ya mwaka wa fedha 2021/22 hivyo ni bajeti ya kupongezwa.
Ameongeza kuwa kiwango Cha bajeti hiyo kilichotengwa ni sawa na asilimia 13.6 ya mapendekezo ya bajeti kitaifa hivyo Kwa mujibu wa mapendekezo ya kitaifa,kikanda na kimataifa ni muhimu bajeti ya elimu kuwa walau asilimia 20 ya bajeti ya Taifa.
Ameongeza kuwa Japo bado mahitaji ni makubwa kuhusu elimu ya Tanzania walau bajeti hiyo imeanza kuleta matumaini na haki elimu imependekeza kuongezwa Kwa bajeti ya elimu kufikia Trilioni 7.39 kama ilivyopendekezwa katika mpango wa maendeleo ya elimu ESDP III.
Aidha amesema suala la kufutwa Kwa ada ya kidato Cha Tano na sita Kwa shule za serikali ni jambo ambalo jema ambalo hata shirika hilo linaunga mkono na litaleta unafuu mkubwa Kwa wazazi na wanafunzi ambapo familia nyingi zimekuwa zikishindwa kugharamia elimu za watoto wao hasa Kwa shule za kata hivyo jambo hilo litapunguza mzigo Kwa wazazi na wanafunzi.
"uamuzi huu kama utaendelezwa unatarajia kuwanufaisha takribani wanafunzi 95,000 wa kidato Cha 5 na zaidi ya 60,000 wa kidato Cha sita wanaojiunga na kufanya masomo yao katika shule za umma ambao wengi wao hutokea familia zenye kipato Cha ching" amesema Dkt Kalage.
Pia ameishauri serikali kuongeza kiwango Cha fedha za ruzuku zinazokwenda kwenye shule kutokana na sera ya elimu bila malipo ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango Cha ruzuku kutoka shilingi 10,000 Kwa wanafunzi wa elimu ya msingi mpaka kufikia 25,000 na kutoka 25,000 mpaka 55,000 Kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari Kwa mwaka,kwani mahitaji ya uendeshaji wa shule hizo ni makubwa zaidi ya Fedha walizotengewa.
Kuhusu Nia ya serikali kutoa mikopo Kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya kati na ufundi shirika hilo limesema hatua hiyo ya serikali itatoa fursa Kwa wanafunzi takribani 385,115 wanaomaliza kidato Cha nne na ambao hushindwa kujiunga na kidato Cha tano kutokana na kuwa na ufaulu wa chini kwani wengi wa watoto hao hutoka familia zenye kipato Cha chini.
Aidha ameongeza kuhusu suala la kutumia uimarishaji wa lugha ya kiswahili kama lugha ya usaili katika nyanja mbalimbali hapa nchini ikiwemo Kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira badala ya kiingereza ni suala jema ambalo litakuza matumizi ya lugha ya kiswahili,na linahitajika kuangaliwa Kwa umakini katika utekelezaji wake.
Pia ameishauri serikali kuwafundisha vyema wanafunzi lugha ya kiswahili Kwa ufasaha ili waweze kuimudu vyema endapo itafundishwa katika ngazi zote za elimu hapa nchini katika kufundisha na kujifunzia kwani hata katika sera ya elimu inaitambua kiswahili kama lugha ya kufundisha.
"Hatusemi kama hakie elimu hatukipendi kiingereza laa ila kiingereza kifundishwe tu kama lugha ya kigeni yaani kama Somo ili pia kuwawezesha wanafunzi kukitumia katika sehemu zenye uhitaji wa lugha ya kiingereza" alisema Dkt Kalage.
- Get link
- X
- Other Apps


Comments