JUKWAA LA KUMBUKUMBU YA HAYATI BENJAMIN MKAPA KUFANYIKA VISIWANI ZANZIBAR MWEZI JULAI.

 JUKWAA LA KUMBUKUMBU YA HAYATI BENJAMIN MKAPA KUFANYIKA VISIWANI ZANZIBAR MWEZI JULAI. 








Dar es salaam. 
Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMF)inatarajia kufanya jukwaa la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama muasisi wa Taasisi hiyo   ambaye pia alikuwa ni Rais wa awamu ya tatu,Hayati Benjamin Mkapa litakalofanyika visiwani Zanzibar mwezi Julai. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam Mbele ya waandishi wa Habari na Afisa Mtendaji mkuu wa Taasisi hiyo,Dkt Ellen Mkondya SENKORO na kuongeza kuwa katika kumbukizi hiyo ya miaka miwili tangu kifo Cha muasisi huyo , kutafanyika mdahalo maalum utakaoangazia masuala  mbalimbali.

Amesema kuwa kauli mbiu ya mdahalo (jukwaa) hilo Kwa mwaka huu ni 'uongozi madhubuti Hamasa ya mabadiliko Kwa wote' ambapo miongoni mwa mada zitazojadiliwa ni pamoja na kuongeza Kasi katika mikakakati ya mabadiliko katika mifumo ya Afya Tanzania kupitia biashara ushirika pamoja na mada ya ubunifu katika miradi na mikakati ya ushirikiano kati ya serikali, Taasisi za umma na za  binafsi katika kuleta huduma ya afya Kwa wote.

"ndugu waandishi wa Habari kupitia mada hizi washiriki watapata fursa ya kusikia mijadala ya juhudi za mashirikiano ya serikali ya Tanzania bara na Visiwani, sekta binafsi na wadau wa maendeleo na pia iliyoendelea kuchagizwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa, katika kuimarisha mifumo ya afya Kwa lengo la kuhakikisha kila mtu popote alipo, anapata fursa ya kupata huduma bora za afya" aliongeza Dkt Ellen SENKORO 

Aidha ameongeza kuwa kupitia mdahalo huo wa siku mbili utakaofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Julai 13-14,2022 na kuhusisha zaidi ya wageni waalikwa 500 utafunguliwa na makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud na siku ya kilele yaan Julai 14 mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mbali na viongozi hao pia viongozi wengine wa kitaifa watakaoshiriki ni pamoja na Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Dkt Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni "msarifu" wa Taasisi hiyo aliyerithi nafasi ya Hayati Benjamin Mkapa kuanzia desemba 2021,pamoja na viongozi wastaafu wa nchi, mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, mashirika ya kimataifa, viongozi wa dini, asasi za kiraia pamoja na marafiki na wanafamilia ya Benjamin Mkapa kutoka ndani na nje ya nchi. 



Hata hivyo,Kwa upande wake meneja tathmini na ufuatiliaji miradi wa Taasisi hiyo,Rahma Musoke amesema mpaka sasa Maeneo karibu yote ya Tanzania yamefikiwa na miradi ya uboreshaji utoaji wa huduma ya afya inayoendeshwa na taasisi kupitia wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo watumishi wa afya zaidi ya 10000 ambao wamepelekwa katika vituo mbalimbali vya afya nchini hasa maeneo ya vijijini, sambamba na kujenga zaidi ya nyumba 482 katika mikoa zaidi ya 12 nchini za watumishi hao wa afya na kufanya marekebisho katika vituo mbalimbali vya afya,

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo pia imetoa ufadhili wa masomo "scholarship" Kwa zaidi ya wanafunzi 900 wanaosoma masuala ya afya ambao wamenufaika na miradi inayoendeshwa na Taasisi. 

Comments