KAMPENI YA UBUNGO YETU,FAHARI YETU YALETA MANUFAA , DC KHERRY JAMES ATAKA USHIRIKISHWAJI WANANCHI.

 

KAMPENI YA UBUNGO YETU,FAHARI YETU YALETA MANUFAA , DC KHERRY JAMES ATAKA USHIRIKISHWAJI WANANCHI. 

Na Mwandishi wetu,Dar es salaam.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Kherry James leo ameizindua kampeni maalum ya kuhamasisha ulipaji kodi na ushuru kwa hiari katika Halmashauri hiyo inayojulikana kama ‘Ubungo Yetu Fahari Yetu’

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo Herry James amesema kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo “tunajenga Ubungo bora,tuitakayo kwa ada,ushuru,tozo na kodi zetu” itasaidia Halmashauri hiyo kupata walipaji wengi zaidi wa kodi,tozo na ada itachochea maendeleo katika Halmashauri hiyo ambayo yatatokana na kodi hizo.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo iliyoanza takribani mwezi mmoja uliyopota imekuwa ni kampeni fanikishi huku akiipongeza idara ya Biashara na kitengo Cha Habari Cha Halmashauri hiyo Kwa kubuni kampeni hiyo ambayo ndani ya mwezi mmoja imefanya Halmashauri ya Ubungo kuwa na ziada ya zaidi ya shilingi bilioni 1.

“Tumezindua kampeni hii tukiamini ni platform nzuri ya kupokea maoni,ushauri wa wafanyabiashara Kwa kihakikisha wanashiriki kulipa kodi vyema na Kwa hiari na leo hii naona pia katika kampeni hii mmeshirikisha na wanafunzi nimefarijika sana Kwa sababu wanafunzi wakielewa umuhimu wa kulipa kodi hii itajenga Taifa lililo imara na viongozi bora wa la baadaye ambao watakuwa wahamasishaji wazuri wa kulipa kodi,tozo na ushuru”alisema mkuu huyo wa wilaya ya Ubungo.

Kampeni hiyo ishirikishe zaidi maoni ya wananchi ili Kwa pamoja gurudumu la maendeleo kwani wananchi walio wengi huwaona maafisa kama maadui pindi waendapo kwenye biashara zao hivyo kampeni hiyo pia itatoa ushauri Kwa wafanyabiashara hao juu ya uendelezaji wa biashara.

Aidha amesema hapendezwi kuona wafanyabiashara wa manispaa hiyo wanafunga biashara zao Kwa kushindwa kujiendesha au kusumbuliwa na watu wa Halmashauri Bali atafurahi kuona biashara zinaendelea na wafanyabiashara hao wanaendelea kulipa kodi Kwa kuona kuwa ni wajibu wao wa msingi katika kulijenga Taifa Kwa pamoja hivyo amewataka maafisa biashara kuendelea kuwa na morali ya kampeni hiyo hata baada ya kumalizika.

Amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa pia kushiriki kikamilifu katika ulipaji wa kodi.

Naye Afisa biashara wa Halmashauri hiyo Peter Ngoti amesemaTimu maalum ya kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa hiari wa kodi bila kishuritishwa imeshaleta matumaimi Kwa wafanyabiashara.


Kampeni imesaidia katika kujenga mahusiano mazuri na rafiki kati ya mafisa wa Halmshauri hiyo na wafanyabiashara ambapo wamewapa link mbalimbali ambazo wafanyabiashara hao wanaweza kutoa kero zao pindi zinapotokea.


Pia kampeni imeongeza mapato ya Haashauri kwani wametoa elimu Kubwa Kwa wafanyabiashara ambao wengi wamelipa kodi na kufanya wigo wa walipa kodi kuongezeka alisema Afisa biashara huyo.


Naye Mfanyabiashara kutoka katika stendi ya Magufuli Terminal,Mbezi louis,Robert Minja amesema kupitia kampeni hiyo yeye kama Mfanyabiashara ameweza kulipa kodi na tozo Kwa urahisi kabisa bila bughdha na pia wamepata njia ya kufikisha malalamiko yao Kwa serikali juu ya kuachana na suala la kamatakata Kwa wafanyabiashara walioshindwa kulipa kodi zao Kwa wakati.

Hata hivyo mbali na kampeni hiyo ya ulipaji kodi wa hiari pia Halmashauri ya Ubungo imetoa vitabu 500 ambavyo vitagawanywa Kwa wanafunzi katika shule mbalimbali wilayani humo ambavyo vitawajengea hari na elimu ya umuhimu wa juu ya ulipaji kodi Kwa hiari Kwa wanafunzi ambao ambao ni walipa kodi na viongozi wa baadaye katika Taifa.











Comments