Mke wa Prof Jay awashukuru Watanzania
Mke wa Prof Jay awashukuru Watanzania
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2022/06/WhatsApp-Image-2022-06-14-at-12.47.30-PM.jpeg)
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa: “Kwa niaba ya Familia ya Joseph Leonard Haule (Prof. Jay) Tunamshukuru Mungu muweza wa yote kwa kuendelea kuiimarisha Afya ya Prof. Jay siku hadi siku mpaka leo.
Kwa Upekee Kabisa Tunamshukuru Rais wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan Kwa kutoa tamko la Serikali yake kugharamia gharama zote za Matibabu ya Joseph Haule (professor Jay ) tunashukuru sana sana na sisi Kama Familia hatuna cha kumlipa bali tunamuombea Kwa Mwenyezi Mungu azidi kumbariki Rais wetu pamoja na Serikali yake 🙏🏽 .
Tunamshukuru Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete @jakayakikwete.
Tunaushukuru Uongozi, Madaktari pamoja na Wauguzi wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili @muhimbili_taifa , Lugalo na Kitengule.
Tunalishukuru Bunge la Tanzania @bunge.tanzania chini ya Spika Dr. Tulia Ackson @tulia.ackson , Viongozi wakuu Chadema na CCM pamoja na wanachama wake wote, kuweka itikadi ya Vyama pembeni na kushughulikia afya ya Prof. Jay mpaka hii leo.🙏🏽
Tunashukuru Wizara mbalimbali haswa Wizara ya Afya @wizara_afyatz (Ummy Mwalimu) @ummymwalimu ,Kwa jitihada mlizozionyesha Kwa kuhakikisha Joseph anapata matibabu ya uhakika, Wizara ya Sanaa @wizara_sanaatz (Mohamed Mchengerwa) Kwa endelea kumtambua Kwa mambo mbali mbali yaliyo kuwa yakiendelea pamoja na kuwa amelala kitandani 🙏🏽.
Tunawashukuru Viongozi mbalimbali wa Dini zote Kwa kujitolea kumuombea sana Joseph bila kuchoka .
Vilabu vya Soka kama Simba , Yanga na vilabu vingine. @simbasctanzania @yangasc
Tunavishukuru pia Vyombo vyote vya habari (TV, Radio na Online media) @cloudstv @cloudsfmtz @wasafitv @eastafricatv na vingine vingi.
@malisa_gj you’re the best 🙌🏽
Bila kuwasahau wananchi wote wa Tanzania ndani na nje ya Tanzania ambao wamekuwa wakimuombea na kumtakia kila lakheri aweza kurudi Sawa 🙏🏽
Mwisho Tunawashukuru Ndugu, Jamaa, Marafiki na Mashabiki wote wa Profesa Jay kwa kumuombea Jay kila siku bila kuchoka. Mungu awabariki sana hatuna cha kuwalipa.🙏🏽🙏🏽
#jaytunakuzimia
ChanzoBongo5
Comments