OSCAR OSCAR,DINA MARIOS WAREJEA E-FM,WAJA NA KIPINDI KIPYA ‘JIONI YA LEO’

 

OSCAR OSCAR,DINA MARIOS WAREJEA E-FM,WAJA NA KIPINDI KIPYA ‘JIONI YA LEO’

Dar es salaam.

Kama wewe ni mtu mitandaoni basi lazima utakuwa umekutana na taarifa juu ya watangazaji wa radio E fm na Tv E,Finna Mario’s na mchambuzi nguli wa soka hapa nchini,Oscar Oscar kuachana na radio hiyo huku viongozi na Wafanyakazi  wa radio hiyo wakiandika mitandaoni Kwa masikitiko juu ya kuondoka Kwa watangazaji hao.


Sasa taarifa ikufikie kuwa watangazaji hao Wala hawakuwa wameacha kazi kwenye radio hiyo Bali ilikuwa ni kama promo ya kipindi Chao kipya ambacho kitarushwa na radio hiyo kuanzia saa 10 mpaka saa 1 usiku.



Kipindi hicho kipya kiitwacho “JIONI YA LEO” ambacho ni mbadala wa kipindi cha UBAONI ambacho hakitakuwepo tena redioni hapo kitawakutanisha Kwa  pamoja Dinna Marios, Oscar Oscar, Mpoki, Roman Shirima na Veronica wa simulizi.


Oscar Oscar ambaye kitaaluma ni mwalimu wa secondari ambaye mwaka huu atahitimu kozi yake ya uandishi wa habari, chuo kikuu Cha Dar es salaam pamoja na Dinna Marios ni wazi sasa Kwa mara ya kwanza wataanza kusikika katika kipindi hicho kipya Cha “JIONI YA LEO”

eFM TanzaniaeFM Tanzania – Muziki InaongeaMuziki Inaongea E-Fm Radio.

Comments