Skip to main content

RC MJEMA ATAKA HALMASHAURI NA MANISPAA SHINYANGA KUANDAA SEMINA KWA WATUMISHI

 

RC MJEMA ATAKA HALMASHAURI NA MANISPAA SHINYANGA KUANDAA SEMINA KWA WATUMISHI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga So/phia Mjema akizungumza kwenye kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kujadili taarifa ya CAG.

NA MWANDISHI WETU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ametoa wito huo wakati alipokuwa mgeni Rasmi kwenye kwenye kikao Maalumu Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika kujadili Taarifa ya na Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha 2020/2021

Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga  imepata hati safi katika majibu ya ukaguzi yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Ambapo Rc Mjema Amesema upo umuhimu mkubwa wa kuhakikisha inaandaliwa semina Maalumu kwa ajili ya watumishi wa Idara mbalimbali pamoja na wale wanaokuwa maalumu katika kuandaa hoja na kuziandika ili semina hiyo iweze kuwapa uwezo zaidi wa kufafanua hoja wanazoziandika na sio wanapotakiwa kutetea hoja hizo hujikuta wakishindwa au Kutoa maelekezo ambayo hupelekea ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali kuwa na wasiwasi juu ya hoja husika

Hata hivyo amewataka watendaji wa Halmashauri katika kikao hicho au hata wanapotakiwa kujibu hoja basi wawe wanajibu vizuri hoja za CAG ili kupunguza wingi wa hoja, sababu baadhi ya hoja zinatokana kwa kutojibiwa vizuri.

"Tunataka halmashauri zetu ziendelee kupata hati safi, lakini hoja ziwe chache na kufutika," amesema Mjema.

Katika hatua nyingine, amemugiza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuhakikisha anasaidiana yeye na Kamati yake ya Ulinzi ya wilaya katika kuhakikisha baadhi ya watu na watumishi wa Serikali ambao walifanya ubadhilifu wa fedha kwenye miradi na kukimbia au kuhama wasakwe popote walipo ili wachukuliwe hatua na kama swala hili likishindikana ngazi ya wilaya basi lipandishwe kwenye ngazi ya Mkoa na yeye mwenyewe kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi watahakikisha wanapatikana na kufikishwa kwenye Mamlaka zinazohusika ili  kufuta hoja za CAG juu ya miradi hiyo.

Manispaa ya Shinyanga ilikuwa na hoja 79, ambazo zilikuwa zimeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo kati ya hoja hizo imejibu 38.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amebainisha hayo leo Juni 25,2022, kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya CAG.

Amesema Manispaa ya Shinyanga katika majibu yaliyotolewa na CAG, baada ya kujibu hoja 38 zilizoibuliwa katika mwaka huo wa fedha (2020/2021) unaoishia Juni 30 imefanikiwa kupata hati safi.

"Majibu ya utekelezaji wa hoja za ukaguzi kama zilivyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),kwa kipindi kinachoishia juni 30, 2021 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tumepata hati safi," amesema Satura.

"Manispaa ya Shinyanga ilikuwa na hoja 79, hoja ambazo zimejibiwa na kufungwa ni 38, na hoja 41 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji," ameongeza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka watendaji wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, kutunza nyaraka za miradi wakati wa manunuzi, pamoja na kupeleka pesa benki za makusanyo ya mapato ili kupunguza hoja.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani, wamesema baadhi ya hoja ambazo zimekuwa zilijirudia mara kwa mara zifanyiwe kazi na kufutwa.

Comments