Skip to main content

RC MJEMA AWATAKA MADIWANI KAHAMA KUTOFUMBIA MACHO DOSARI, FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.

RC MJEMA AWATAKA MADIWANI KAHAMA KUTOFUMBIA MACHO DOSARI, FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO. 



Kahama,SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amewataka Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa Kahama kutosita kuhoji pale watakapobaini dosari yoyote katika maendeleo au fedha za Miradi zisipo tumika ipasavyo

Rc Mjema ametoa wito huo wakati wa kikao maalumu  Cha baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kikao hicho ambacho kilikuwa na jumla ya hoja 87 huku kukiwa na hoja 60 ambazo Manispaa hiyo tayari   imezifanyia kazi na kufungwa na jumla ya hoja 27 bado utekelezwaji wake unaendelea

Mhe. Mjema amesema Manispaa hiyo ya Kahama imejitahidi katika kupunguza wingi wa hoja ambazo zilipelekea kuwa na Idadi ndogo ya hoja tofauti ambazo ziliwasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali huku akitoa agizo la kuhakikisha ifikapo tarehe 15/07/2022 hoja zote zinazopaswa kushughulikiwa ziwe zimetatuliwa na kufungwa 

Aidha ameongeza kuwa endapo Madiwani wasipokuwa makini katika kuhoji matumizi ya fedha zote ambazo zinatolewa na Serikali wataisababishia Manispaa hiyo kuwa kwenye mtiririko wa hoja nyingi na baadae kupelekea kupata hati chafu ' Nawapongeza Madiwani kwa kuwa makini katika kuhoji matumizi sahihi ya fedha zote ndani ya Manispaa yenu sawa mara kwa mara mnapata hati Safi Sasa muendelee hivyo hivyo na mjitahidi kusiwepo na hoja kabisa' amesema Rc Mjema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga amesema Manispaa ya Kahama imekuwa ni Moja ya Manispaa katika Mkoa wa Shinyanga ambayo ina vyanzo vingi vya mapato na jukumu walilonalo ni kuhakikisha wanasimamia vyema vyanzo vyote vya mapato ili kutotegemea fedha nyingi toka serikali Kuu

Kwa upande wake Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa Kahama Bwn. Anderson D.Msumba amesema Manispaa hiyo imejipanga  kuhakikisha inatekeleza maoni na ushauri uliotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Comments