SHIRIKA LA AGENDA LASHAURI NCHI ZA KIAFRIKA KUPAMBANA NA KEMIKALI HATARISHI,MATUMIZI YA BIDHAA ZA PLASTIKI.
SHIRIKA LA AGENDA LASHAURI NCHI ZA KIAFRIKA KUPAMBANA NA KEMIKALI HATARISHI,MATUMIZI YA BIDHAA ZA PLASTIKI.

Na Thadei PrayGod
Dar es salaam
Imeelezwa kuwa utafiti uliofanywa hivi karibuni umebaini kuwa bidhaa nyingi za plastiki kama vile midoli na zile zilizotengenezwa kutokana na plastiki iliyorejelezwa na kuuzwa katika nchi za Afrika na Uarabuni zina viwango vikubwa vya sumu ya kemikali zinazozalishwa bila kukusudia.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam,Afisa Programe Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali hapa nchini la AGENDA,Silvani Mng’anya amesema kuwa utafiti huo umefanywa na maabara huru nchini Jamhuri ya Czech ambapo umebaini vifaa vingi vya plastiki kama vile midoli,vifaa vya Jikoni,ofisini,vitana na vibanio vya nywele na vifaa vingine vilivyorejelezwa vina viwango vikubwa vya kemikali hiyo.
Amesema kubwa kulingana na ripoti mpya ya utafiti ulifanyika kwa sampuli mbalimbali kutoka nchi 9 za Afrika na 2 za Uarabuni na kutolewa na na asasi ya Arnika pamoja na mtandao wa kimataifa wa IPEN ambapo imebainika kuwa bidhaa 61 zitokanazo na plastiki zina kemikali ambazo huzuia muwako wa moto na kemikali ya dioxin zinazodumu kwenye mazingira Kwa muda mrefu.
Aidha ameongeza kuwa kwa kujibu wa tafiti nyingi zimehusisha kemikali hizo na magonjwa mbalimbali ikiwemo Kansa,kuathiri ukuaji wa ubongo kwa watoto,ugumba na utasa na matatizo mengine ya kiafya Kwa wanadamu na zimepigwa marufuku kwenye mkataba wa kimataifa wa Basel.
"Kemikali za kuzuia muwako wa moto kwenye bidhaa za plastiki(Brominated Flame Retardants BFRs)na kemikali sumu nyingine zinazozalishwa bila kukusudia (dioxins)hazipaswi kuwepo kwenye midoli ya kuchezea watoto pamoja na kwenye bidhaa za plastiki za nyumbani”alisema Afisa program huyo mkuu wa Agenda.
Aidha ameongeza kuwa kemikali hizo za dioxin athari yake inaweza kuwa na madhara sawa kama Yale yatokanayo na taka hatarishi.
Hata hivyo AGENDA wamependekeza kuwa viwango vya ukomo vya chini vya POPs vitumike kukomesha taka za ki-elektroniki pamoja na vifaa vya plastiki vitokanavyo na Magari yaliyokwisha muda wake kutumika katika kurejelezwa Kwa ajili ya kuunda bidhaa mpya.
Pamoja na taka za ki-elektroniki na vifaa vya Plastiki kutoka kwenye Magari yaliyokwisha muda wake (ELVs)yenye viwango vikubwa vya kemikali sumu za kuzuia mwako wa moto zinapaswa kuzuiwa kuingia katika mnyororo wa urejelezaji ili kukomesha kabisa uingiaji wake Kwa kufuata mkataba wa kimataifa wa Basel,
Sambamba na kuorodheshwa kemikali ya Brominated dioxin kwenye orodha ya kemikali za POPs zinazozalishwa bila kukusudia zinosimamiwa na mkataba wa kimataifa wa Stockholm.
"Kemikali hizi za Brominated dioxin zilionekana katika sampuli nyingi zilizofanyiwa uchunguzi,viwango vyake katika chakula na bidhaa nyingne ni vikubwa na vinaogopesha,na hivyo kuonyesha vinahitaji mwongozo wa kimataifa kama kemikali nyingine za POPs za kundi la klorini ambazo zimeorodheshwa katika kiambatanisho C Cha mkataba wa kimataifa wa Stockholm” aliongeza
Hata hivyo ameongeza wao kama moja ya shirika lililopo katika makundi ya watetezi wa mazingira wametoa wito Kwa nchi za Afrika kuweka vikomo zaidi Kwa bidhaa za plastiki zinazotengenezwa Kwa plastiki zilizorejelezwa.


Comments