Skip to main content

TAA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII WAINGIA MAKUBALIANO KUWEZESHA MACHINGA

 

TAA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII WAINGIA MAKUBALIANO KUWEZESHA MACHINGA





CHAMA cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimesaini makubalianono (MoU) na Wizara ya Maendeo, Jinsia, Wazee, Wanawake na Makundi Maalum ili kurasimisha biashara za wamachinga na bodaboda nchini.

Akizungumza leo Juni 20, 2022 jijini Da es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubalianono hago, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameipongeza TAA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi pamoja na wamachinga.

Amesema jambo hilo litasaidia kuhakikisha Wafanyabiasbara hao wanaimarika na hivyo kukuza kipato chao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Lengo la Serikali ni kuwa na mfumo na utaratibu wa kuwasimamia Wafanyabiashara hawa na hatimaye wawe wakubwa zaidi,” amesema Mpanju na kuongeza,

“Hivyo tunaingia makubaliano haya ili waweze kuwezeshawa, Wakati tukiendelea kuboresha mfumo bora wa kuwasimamia kuanzia ngazi ya Kata hadi Taifa,”.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TAA Victorius Kamuntu amesema kama wataalamu wameamua kuingia makubalianono hayo ili kuhakikisha wanawezesha Makundi hayo Maalum.

“Sisi tunalenga ni namna gani watu wa chini wanaweza kuwezeshawa na kukuza biashara zao. Tunaamini tukiungana kwa pamoja tuna uwezo wa kukuza uchumi wa nchi, “ amesema Kamuntu.

Aidha amesema wao kama wataalamu watatumia fursa hiyo kuwashauri ni namna gani wanaweza kuwa wakubwa.

Credit...darubini ya habari

Comments