TAMASHA LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM LAFANYIKA,SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZAO.M

 TAMASHA LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM LAFANYIKA,SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZAO.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe akiwa kwenye picha pamoja na moja ya watoto wenye mahitaji maalum.



 Dar es salaam.

 Serikali imeahidi kuendelea kusimamia haki za watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwatatulia changamoto mbalimbali


Hayo yamesemwa na MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe wakati akizungumza kwenye tamasha la watoto wenye mahitaji maalum ambalo limefanyika katika kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama jijini Dar es salaam lenye kauli mbiu isemayo “Haki sawa kwa wote” lililoandaliwa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania.


Tamasha hilo limewakutanisha kwa pamoja watoto wenye mahitaji maalum kwa pamoja ambapo wameshiriki michezo mbalimbali,ngoma pamoja na shughuli nyinginezo na pia limewajengea uelewa.


.

Gondwe amesema kuwa wao kama  Wailaya ya Kinondoni wamekuwa wakitoa huduma kwa makundi Maalum katika kuwawezesha kiuchumi ili waweze kuendesha maisha yao sambamba na kuwasaidia.


“ Serikali inatoa fedha kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wanawake, vijana pamoja na watu wenye mahitaji Maalum ili waweze kujikomboa kiuchumi. Mfano kwa mwaka 2022 tumetoa shilingi 255,425,000, zote hizi ni juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapatiwa huduma bora kwa usawa bila kujali umri, Jinsia au maumbile,”alisema Mkuu huyo wa wilaya 


Aidha ameongeza kuwa pamoja na mambo Mengi mazuri ambayo wanayafanya kwa watu wenye mahitaji Maalum wakiwemo watoto,lakini bado kuna changamoto ambazo familia pamoja na watu wenye mahitaji Maalum wanazipitia.

Akizitaja changamoto hizo DC Gondwe amesema  kuwa ni pamoja na hali duni za maisha ya familia zenye watoto wenye mahitaji Maalum na hivyo wengine kupelekea kuingizwa kwenye biashara za kuombaomba na watu wasio na mapenzi mema na watoto hao ili kujipatia fedha jambo ambalo wilaya ya Kinondoni haikubaliani nalo


Hata hivyo DC Gondwe ametoa wito wanaofanya ukatili wa namna yoyote ile kwa watoto hao kaucha mara moja kwani sheria zipo watashughulikiwa ipasavyo pindi watakapobainika ikiwemo kuchukuliwa hatua za kisheria

Afisa ustawi wa jamii, Makumbusho ya Taifa Wilhelma Joseph akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii, Makumbusho ya Taifa Wilhelma Joseph amesema tamasha hilo limejukuisha watoto wenye mahitaji Maalum wakiwemo wenye uoni hafifi, walemavu wa ngozi na wengine wenye mahitaji Maalum.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuwaweka pamoja na kuweza kushirikiana kwa pamoja watoto hao wenye mahitaji maalum na wale wasio na mahitaji maalum na kuongeza kubwa kauli mbiu ya tamasha hilo ambayo ni haki sawa kwa wote imeakisi uwepo wa tamasha hilo.


Amesema watoto waliojumuika pamoja ni kutoka katika vituo vya kuelekea watoto hao pamoja na shule zenye watoto wenye mahitaji Maalum.

Katika tamasha hilo watoto wenye mahitaji maalum wa shule mbalimbali jijini Dar es salaam wameshiriki ikiwemo waliotoka katika shule za Jeshi la Wokovu, (kurasini)Shule ya msingi Mugabe(Sinza) Uhuru Mchanganyiko,(Ilala)Shule ya msingi Sinza, Shule Msingi Makumbusho na Mikocheni.

Mtoto mwenye mahitaji maalum akiimba katika tamasha la watoto wenye mahitaji Maalum,katika kijiji cha Makumbusho ,Kijitonyama

Comments