WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO OPERESHENI YA ANUANI ZA MAKAZI

 WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO OPERESHENI YA ANUANI ZA MAKAZI

Screenshot_20220619-125619_Chrome


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zote zenye dhamana ya masuala ya ardhi na makazi kuhakikisha zinakuja na mikakati thabiti ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi iliyoainishwa wakati wa utekelezaji wa zoezi la operesheni ya anuani na makazi.


Ametoa wito huo Jumamosi Juni 18, 2022 wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la operesheni ya anuani na makazi, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.


“Pia toeni miongozo ya namna bora ya kushughulikia changamoto za Watanzania wenzetu kuishi katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria Ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika na fursa zitokanazo na zoezi hili”.


Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi katika ngazi zote hususan kwenye Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utunzaji wa mifumo sambamba na kulinda miundombinu ya anwani za makazi kwenye maeneo yao.


“Viongozi na Watendaji hakikisheni kuwa jamii inaendelea kuelimishwa ili kujua manufaa sanjari na kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa anwani za makazi katika maeneo yao”.


Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara zote, Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa kuendelea kushughulikia changamoto zote zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni anwani za makazi na kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu.


“Mpango wa Uendelezaji wa Mfumo (System Sustainability Framework) unaotoa mwongozo wa shughuli zote za anwani za makazi zitakavyofanyika utumike vizuri ili kufanya zoezi hili kuwa na thamani wakati wote”

Comments