ACT WAZALENDO YAIKALIA KOONI KAMPUNI YA TICTS, YAISHAURI SERIKALI ‘KUIPIGA CHINI

 

ACT WAZALENDO YAIKALIA KOONI KAMPUNI YA TICTS, YAISHAURI SERIKALI ‘KUIPIGA CHINI’


Dar es salaam. 

Chama Cha ACT WAZALENDO kimeishauri Serikali kuendelea kuboresha usimamizi wa bandari Kwa kutozipa zabuni kampuni ambazo haziwezi kuleta mapinduzi katika sekta ya uchukuzi. 


Msemaji wa sekta ya mawasialiano,teknolojia ya Habari na uchukuzi na  Ally Salehe amesema Utendaji kazi wa kampuni binafsi ya kuhudumia makontena TICTS siyo wa kuridhisha  ambapo wadau wameishauri serikali kutoipa tena kampuni hiyo mkataba mpya wa kuendelea kufanya kazi zake hapa nchini.


Amesema lengo la serikali kuipa mkataba kampuni hiyo lilikuwa jema na la kupongwezwa lakini kama kampuni imeshindwa kutekeleza mkataba huo Kwa kuchangia kuchelewesha ushushaji wa mizigo na makontena kukaa zaidi bandarini. 


ACT inaamini dhima ya serikali ni kuchochea maendeleo Kwa kuwekeza kwenye mashirika ya umma ili kukuza uchumi Kwa madhumuni ya kupata mapato,kusogeza na kutoa huduma Kwa urahisi Kwa jamii na kuchochea maendeleo  katika sekta ya umma pamoja na sekta mbalimbali za uchumi lakini Kuna baadhi ya makampuni yanaikwamisha serikali katika harakati zake kuinua uchumi.


Serikali kufanya uchambuzi wa kina Kwa kutoa zabuni Kwa kampuni zenye sifa za kimataifa Kwa kuipima TICTS katika utendaji wake hapa nchini wa zaidi ya miaka 20 ili kuwapo na mkataba bora.

Serikali ianze mchakato wa kutafuta kampuni nyingine na shughuli ilizokuwa ikifanya kampuni hiyo zisimamiwe na Kwa muda na mamlaka ya bandari hapa nchini TPA.

 

“Sisi ACT WAZALENDO tunaungana na wadau wengine kuwa suala la ukodishwaji au kutokodishwa tena  TICTS lichukuliwe na lifanyiwe maamuzi katika hali ya uzalendo mkubwa Kwa maana ya kujali maslahi ya Taifa”alisema Ally Salehe


Aidha ameongeza kuwa ni vyema Kwa serikali sasa kuongeza ufanisi mkubwa katika bandari Kwa kuisimamia Kwa umuhimu mkubwa ili kuongeza tija na ufanisi wake. 

Comments