CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR, (SUZA) CHAJIVUNIA KUZALISHA WATAALAMU KATIKA NYANJA MBALIMBALI.

 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR, (SUZA) CHAJIVUNIA KUZALISHA WATAALAMU KATIKA NYANJA MBALIMBALI. 

JINSI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU HURIA CHA

Makamu mkuu wa chuo kikuu Cha Taifa cha Zanzibar SUZA aliyesimama katika akiwa katika picha ya pomoja mbele ya Banda la chuo na baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali za chuo hicho katika uwanja wa mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam. 
Makamu mkuu wa chuo, chuo kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA)Prof. Moh'd Makame Haji Akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Banda la chuo hicho katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam. 

Na Thadei PrayGod

Chuo kikuu Cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)kimesema kuwa kitaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu Kwa kutengeneza rasilimali watu Kwa kutoa wataalamu watakaoshiriki katika harakati za kuleta maendeleo ya Taifa.


Hayo yamesemwa na makamo mkuu wa chuo hicho Profesa Moh'd Makame Haji alipokuwa Akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Banda la chuo hicho kinachoshiriki Katika maonesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu TCU.

Prof Haji amesema kuwa kozi za fani zinazotolewa katika chuo hicho huangalia zaidi Maeneo ambayo yatakuwa na uwezo wa kutengeneza vijana na wataalamu kuweza kujiajiri pamoja na kuangalia namna ambavyo wanaweza kutumia  vipaji vyao kwenye kuwekeza katika vitu vitakavyotokana na ubunifu wao wenyewe. 

Amesema kuwa chuo hicho hutoa elimu kupitia kozi mbalimbali katika ngazi za afya, elimu, sayansi jamii, sayansi asili, biashara, uchumi, Fedha pamoja na kozi za utalii.

Akizitaja kozi nyingine zinazotolewa na chuo hicho amesema kuwa ni pamoja na kozi za sayansi za bahari pamoja na kozi za lugha ikiwemo lugha ya kiswahili. 

Aidha ameongeza kuwa chuo hicho pia kimekuwa kikifanya shughuli mbalimbali za kitafiti Kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani ya nchi na nje ya nchi vikiwemo vyuo vikuu na Taasisi nyingine za elimu na utafiti.

"ndugu wanahabari chuo Cha kikuu Cha Taifa cha Zanzibar SUZA pia tumekuwa tukitoa ushauri elekezi kwa Taasisi mbalimbali ikiwemo za serikali na hata zile za binafsi kama chuo Cha Taifa ambacho kinamilikiwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambacho mkuu wake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ambaye Kwa dhati kabisa anawekeza nguvu zake zote kuhakikisha kuwa chuo kinafanya kazi vizuri na kinatoa huduma zake katika mazingira yaliyo mema na mazuri bila kusahau maadili mema Kwa wote wanaopita katika chuo chetu"Alisema Profesa Moh'd Makame Haji.

Ameongeza kuwa chuo hicho pia kinaangalia sera kuu za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na zile za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza kukuza lugha ya kiswahili ikiwemo kufundisha fani hiyo Kwa wageni wa nje ya nchi pamoja na wataalamu wa ndani ya nchi kuanzia ngazi za cheti,diploma hadi ngazi ya shahada za uzamivu (PhD) na kimehakikisha lugha ya kiswahili italeta manufaa ulimwenguni kote.

"SUZA tuna kituo maalum Cha kuangalia uboreshaji wa lugha ya kiswahili ambapo tunafanya tafiti na kukusanya wataalamu Mbalimbali Kwa kuandaa makongamano,kutayarisha vitabu na vitini vinavyotumika kufundisha na kujifunzia lugha ya kiswahili na wataalamu wetu wanafanya kazi na serikali zote mbili kuhakikisha kwamba lugha yetu ya kiswahili inapanua na kufungua mbawa zake Kwenda ulimwenguni kote"aliongeza makamo huyo mkuu wa chuo.

Hata hivyo amewataka walezi na wazazi kutembelea Banda la chuo hicho na kuwapeleka vijana wao kujiunga na chuo hicho kikuu Cha Cha Taifa Zanzibar SUZA kwani kinatoa elimu bora Inayozalisha wataalamu bora katika nyanja na fani mbalimbali wakiwemo watafiti, wanasayansi na wataalamu wengine kuendana na sera ya chuo hicho isemayo "kichocheo Cha mabadiliko ya jamii kwani wako tayari katika kubasilisha jamii kuwa jamii bora yenye mwelekeo wa kitaaluma kupitia elimu.

Chuo kikuu Cha Taifa Zanzibar SUZA ni moja ya vyuo vinavyoshiriki katika maonesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu TCU yaliyoanza Julai 18 hadi Julai 23 mwaka huu. 

Comments