GLOBAL EDUCATIONAL LINK YAJIPA 'MAUJIKO'KUTOA HUDUMA YA KUWAUNGANISHA WANAFUNZI WA TANZANIA NA VYUO VIKUU NJE YA NCHI.

 

GLOBAL EDUCATION LINK YAJIPA 'MAUJIKO'KUTOA HUDUMA YA KUWAUNGANISHA WANAFUNZI WA TANZANIA NA VYUO VIKUU NJE YA NCHI. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd, Abdulmalik Mollel.
 
 
 Na Thadei PrayGod, Dar es Salaam

Kampuni ya Global Educational Link Ltd inashiriki kwenye maonyesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu TCU yaliyoanza Julai 18 hadi Julai 23 mwaka huu.

Maonyesho hayo huwakutanisha Kwa pamoja vyuo vikuu,Taasisi za elimu,mawakala wa vyuo vikuu nje ya nchi pamoja na wanafunzi wanaotaka kusoma vyuo vikuu nje ya nchi.


Moja wa wakala mkubwa na maarufu wa elimu nje ya nchi ni kampuni ya Global education link ambayo mkurugenzi wake Abdulmalik Mollel amewaambia wanahabari kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki maonyesho hayo mara Kwa mara na imewapeleka mpaka sasa wanafunzi wengi kupata elimu zao nje ya Taifa la Tanzania kupata elimu bora.

Mkurugenzi huyo  amewashauri wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi kunitumia kampuni ya Global education link kwani imekuwa Msaada mkubwa Kwa walezi na wazazi ambao hupendelea kupeleka watoto wao kusoma nje ya nchi katika ngazi za vyuo 

Aidha ameongeza kuwa kampuni hiyo hutoa fursa za masomo zinazopatikana katika nchi za Ulaya ikiwemo Georgia, Cyprus na Uturuki huku akiwataka watanzania kuendelea kutafuta elimu ambayo itaendana na soko la ajira katika uhitaji wa ajira hizo ulimwenguni kote ikiwemo Tanzania.

Hata hivyo amewataka vijana kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi(scholarship)ambazo hutolewa na vyuo vingi nje ya nchi ili kujiendeleza kimasomo. 

Maonyesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu TCU yanaendelea katika Viwanja hivyo ambapo yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 23 mwaka huu. 

Comments