JULAI 7: SIKU YA KISWAHILI DUNIANI,SIKU KUU YA SABASABA
JULAI 7: SIKU YA KISWAHILI DUNIANI,SIKU KUU YA SABASABA
Leo Taifa la Tanzania limepata fursa kubwa na adhimu ulimwenguni huku dunia ikiitambua rasmi tarehe ya leo kama siku ya lugha ya kiswahili duniani.
Upekee wa siku hii ya leo ni pale Taifa linapolenga ndege wawili kwa jiwe moja wooh watu wa mataifa ya magharibi hupenda kusema 'it's great'' kwani leo pia ni siku kuu ya biashara hapa nchuni,ambapo kunafanyika maonyesho makubwa ya kibiashara maarufu kama 77 naam embu tuliweke hilo pembeni kwanza na kurejele katika siku hii adhimu ya kiswahili kwani Tanzania miongoni mwa mataifa yanayoongea lugha hiyo kwa ufasaha zaidi na ni lugha yetu ya Taifa.
Siku hii inalenga kukuza matumizi ya Lugha hiyo kama nguzo ya Umoja, Ustawi na Amani
#Kiswahili ni miongoni mwa Lugha zinazotumiwa zaidi Afrika, na kwa Mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) ni kati ya Lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi duniani, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya Milioni 200
Tukirejea katika siku ya 77 ni kwamba,
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika.Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.
Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo, Bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi. Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara.
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere yaani viwanja vya sabasaba.



Comments