MANARA ALAMBA DILI NONO,UBALOZI WA BAYPORT.

 MANARA ALAMBA DILI NONO,UBALOZI WA BAYPORT.




Na mwandishi wetu,

Dar es salaam,Msemaji wa klabu ya Yanga,Haji Sunday Manara leo ameingia mkataba na taasisi ya kifedha ya BayPort Financial Services kama balozi wa taasisi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba huo mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam,Manara amesema kuwa ubalozi huo ni heshima kubwa kwake,kwa klabu yake ya Young Africans pamoja na mpira wa miguu wa Tanzania kwani ilizieleka ni wasanii ndiyo waliokuwa wakipata ubalozi kwenye makampuni mbalimbali.

Amesema kuwa kutokana na kukua kwa soka la Tanzania na kuheshimishwa ndiyo sababu taasisi ya BayPort imempa ubalozi kutokana na ushawishi wake katika soka la Tanzania na jinsi anavyotumia mitandao ya kijamii

Aidha ameongeza kuwa taasisi hiyo ya BayPort inatoa huduma zake kwa mujibu wa kanuni za benki kuu ya Tanzania na kwa kufuata sheria za fedha hivyo amewataka watumishi wa umma kuitumia taasisi hiyo kama sehemu yao ya kupata mikopo ili kupunguza gharama za maisha kwa watumishi hao.

“zamani ilikuwa kupata mkopo mpaka uzunguke huku na huko kuomba mkopo,uandike makaratasi mengi lakini BayPort imekuja na suluhisho la kutoa mikopo kiurahisi kabisa kwa watumishi wa umma kwa kutumia simu ya mkononi hivyo huu ni taasisi mkombozi kwa watumishi wa umma”alisema Haji Manara.

Hata hivyo amewaasa watanzania hususan wachezaji wenye umaarufu kutumia mitandao yao vizuri ili kujipatia kipato zaidi kutokana na shughuli za ubalozi ambazo wanaweza kuzipata.

Naye Ndelingo Mateo afisa uendeshaji wa BayPort amesema taasisi hiyo inayotoa mikopo kwa watumishi wa umma kwa takribani miaka 16 sasa hapa nchini imeamua kumchagua Manara kama balozi wake kutokana na ushawishi wake alio nao ndani na nje ya nchi.

Amesema taasisi hiyo ndiyo taasisi ya kwanza hapa nchini ya kifedha kutoa mikopo kwa njia ya kidigitali ambapo mtumishi wa umma mwombaji hutumia simu yake ya mkononi na baadaye kupata mkopo kiurahisi zaidi.

Akiuzungumzia kampeni ya taasisi hiyo ya BayPort iliyozinduliwa hivi karibuni. (NDIOO)Afisa uendeshaji huyo amesema kuwa ni dhihirisho kuwa wanatoa mkopo kwa haraka zaidi hapa nchini ambapo mtumishi wa umma anaweza kupata mkopo ndani ya masaa 24 tu tena kwa kutumia simu yake ya mkononi.

"ndugu wanahabari sisi kama Bayport ni moja ya taasisi kubwa za kifedha hapa nchini na utoaji wetu wa mikopo ni rahisi kabisa kwani mtumishi yoyote wa umma anaweza kupiga *150*49# na akapata mkopo kwa urahisi zaidi bila kuhangaika ndani ya masaa 24 tu bila hata kuhangaika na makaratasi au kuambiwa njoo kesho,njoo kesho sisi tunakupa mkopo Fasta "alisema Bw Nderingo Materu

Dili hilo la ubalozi wa taasisi ya kifedha ya Bayport limekuja ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la soka Tanzania bara TFF lililotangaza kumfungia msemaji huyo wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara NBC 21/22 Young African Sports Club.



Comments