WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI WATAKIWA KUWAPA MIKATABA MADEREVA KABLA YA MWEZI AGOSTI.

 WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI WATAKIWA KUWAPA MIKATABA MADEREVA KABLA YA MWEZI AGOSTI. 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi.


Na TP,Dar es salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewataka Wamiliki wa vyombo vya Usafirishaji ikiwemo magari yanayosafirisha abiria na Mizigo ya ndani na yale yanakwenda nje ya nchi  kuwapatia mikataba ya kazi  madereva kabla ya mwezi agosti mwaka ambapo serikali itachukua hatua kali kwa watakaoshindwa kutekeleza maagizo hayo ambayo ni takwa la kisheria

Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo leo Dar es salaam katika kikao kazi  kilichohusisha wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo  Wizara  hiyo,wizara ya mambo ya ndani,jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani,makampuni ya usafirishaji,pamoja na wadau wengine mara baada ya  kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri hapa nchin.

Naibu waziri huyo amesema kwamba baada ya wizara hiyo  kupokea malalamiko hayo kutoka vyama vya wafanyakazi madereva miezi mitatu iliyopita na kuahidi kuyashughulikia serikali ilifanya ufuatiliaji  nakubaini Jumla ya Makampuni 73  hayajazingatia takwa la kisheria la kuwataka wamiliki kuwapa mikataba wafanyakazi wao.

Kuhusu madereva wanaosafirisha shehena za mizigo kwenda nje ya nchi amesema kwamba serikali pia imeweka utaratibu Kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha mafuta na gesi nje ya nchi ikiwemo Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo kuwalipa posho kwa kuzingatia utaratibu wa kisheria wa malipo ya siku 20 za kusubiria kushusha na kupakia mzigo kwa dola 10 za kimarekani Kwa  siku sawa na shilingi za kitanzania elfu 23000.

"Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa posho hizi kwa madereva imeshirikisha vyombo vya utatu vinavyohusika kisheria kuishauri Serikali katika suala hili ambavyo ni LESCO na Bodi ya Kima cha Chini cha Mshabara kwa sekta Binafsi na kupokea maoni yao,Maoni hayo ambayo nimeyaridhia ni kiwango cha malipo ya safari ya kwenda na kurudi na mzigo(retuns )kuwa shilingi 330,000 na malipo ya kushusha na kupakua mzigo kuwa dola 170 za kimarekani" amesema Katambi.

Hata hivyo ameyataka makampuni ya usafirishaji kuwaunganisha madereva wao na mifuko ya hifadhi za jamii hapa nchin ikiwemo NSSF na kupeleka makato yao katika mifuko hiyo ili baadaye madereva wawe ni sehemu na wanaopokea mafao baada ya kustaafu kazi zao.

Ameongeza kwa ni lazima pia madereva waunganishwe na kupata bima za afya huku suala la kujiunga na vyama vya wafanyakazi likiachwa kuwa maamuzi ya madereva hao.

 "Kama wizara Nasisitiza viwango hivi vya posho ni sehemu ya mkataba wa hali bora kwa Wafanyakazi Madereva ambavyo vitapaswa kuzingatiwa na waajiri katika Mikataba ya ajira zao"aliongeza waziri huyo.

Pia amesema kuwa serikali itaendelea kufanya kaguzi za kazi ikiwa ni pamoja na kukagua mikataba hiyo kama imezingatia Makubaliano hayo,nakwamba kuhusu utaratibu wa kupakia na kushusha mafuta na gesi, Serikali imetoa Mwongozo wa kupakia na kushusha mafuta wa mwaka 2021 kwa wadau wote wa usafirishaji wa mafuta.

Hata hivyo ameongeza kwa ni  jukumu la kila Mdau kuhakikisha taratibu za upakiaji mafuta zinafuatwa wakati akiwa katika bohari yoyote,serikali itaendelea kutoa elimu kwa wadau wote ili waweze kuzingatia Mwongozo ukiwemo ule wa ubebaji wa mizigo hatarishi zikiwemo kemikali na kusema kuwa makampuni yote yanatakiwa kutimiza maagizo ya serikali na endapo watabainika kukiuka basi sheria itachukua mkondo wake.



Comments