WASTAAFU MKOA WA DAR ES SALAAM WAMIMINIKA KUSIKILIZA KUHUSU HATMA YA MAFAO YAO.

 WASTAAFU MKOA WA DAR ES SALAAM WAMIMINIKA KUSIKILIZA KUHUSU HATMA YA MAFAO YAO. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira ,Vijana na Watu wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akiwasikiliza na kuwahudumia wastaafu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wake wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wastaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam.



Na Thadei prayGod,Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu KaziAjira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amekutana na wastaafu wa mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo ule wa watumishi wa serikali na mashirika ya umma yaan PSSSF pamoja na ule wa watumishi wa sekta na mashirika binafsi NSSF jijini Dar es salaam ili kufahamu changamoto wanazokutana nazo katika madai ya mafao yao kama wastaafu.

Hata hivyo mara baada ya kuwasikiliza wastaafu hao Prof.Ndalichako ameaigiza Mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii PSSSF na NSSF kulipa mafao  kwa wastaafu kwa wakati pamoja na kuhakikisha wanawalipa Wastaafu wote wanaodai mifuko hiyo  ikiwemowanaodai kiinua mgongo,fidia,na waliopunjwa. 

 Waziri Prof Ndalichako amesema lengo lakukutana na wastaafu hao ni kusikiliza malalamiko yao ,ambapo amedai kuwa tangu ameingia kwenye Wizara hiyo takribani miezi sita  amebaini wastaafu wengi wamestaafu  lakini bado hawajalipwa stahiki zao na wanaishi maisha magumu hivyo waje na vielelezo ili wafanyiwe mchakato wa kulipwa.

Wengi wa wastaafu hao walionekana kutaka kufahamu hatma ya mafao yao na kuyasubiri kwa hamu maelekezo ya waziri huyo kwa mifuko hiyo hifadhi za jamii ambayo ambapo waziri huyo amewahakikishia kuwa wataendelea kulipwa mafao yao pamoja na viinua mgongo na wale waliopunjwa malalamiko yao yatashughulikiwa.

Waziri huyo amesema kuwa serikali itaendelea kuthamini mchango wa wastaafu hao kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kulitumikia Taifa katika nyanja mbalimbali na itahakikisha wanaendelea kulipwa mafao yao na stahiki zao ikiwemo viinua mgongo vyao kwa wakati kupitia NSSF na PSSSF.

"Wastaafu hawa wanaodai madai yao wapo katika makundi tofautitofauti ikiwemo mapunjo ambapo mafao ya mtu yamekokotolewa kwa kutumia mshahara ambao ni mdogo kuliko mshahara halisi wa mfanyakazi alipostaafu na kusababisha mafao ya mkupuo anayopewa ni kidogo kuliko ilivyotakiwa"amesema Profesa Ndalichako.

Aidha Waziri Ndalichako ameendela kusema  kwamba wizara hiyo imekuwa ikifuatilia suala la pensheni za wastaafu hapa nchini  ambapo imebaini  kuwepo kwa kesi za wastaafu ambazo  ziko wazi na kwamba suala lililopo  nikwenda tu kurekebishiwa mapunjo yao na kulipwa kwa kuzingatia mshahara wake wa mwisho ,nakusisitiza wastaafu  hao warudishiwe stahiki zao zote walizokuwa wanapunjwa.

Aidha amesema kwamba kuna baadhi ya Wastaafu vikokotoo vyao viko sawa lakini walikuwa hawana Elimu juu ya Vikokotoo hivyo,ambapo wamepatiwa Elimu na kujiridhisha kwamba hawajapunjwa mafao yao.

Kadhalika  Waziri Ndalichako amesema kumekuwa na makosa ya kiutendaji kutoka kwa baadhi ya watendaji wa mifuko ya pensheni kutokusikiliza malalamiko ya wastaafu wanaokuja kudai stahiki zao hivyo ameagiza watendaji hao kuacha tabia hiyo kwani wao ni watishi wa Umma.
 
Kassim Mafanya ni mkaazi wa jiji la Dar es salaam na mstaafu  wa Chuo cha askari  Magereza Ukonga  ambapo amesema anashukuru kupata nafasi kusikilizwa kwani wastaafu wengi wamekuwa wanaishi kwa msongo wa mawazo na maisha yao hayaeleweki hawajui kesho yao  wamekuwa wakiahidiwa kupata nyongeza lakini hakuna kinachoendelea wengine wanafariki bila hata ya kufaidi chochote kutokana na jasho lao.

Kwa upande wake Bi Chuki Kashaija ambaye alikuwa ni  Mtumishi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Chuki Kashaija mwenye ulemavu wa miguu  amesema alianza kazi tangu mwaka 1973 na baadaye alistaafu mwaka 2014,ambapo  amesema mpaka sasa hajapata mafao yake takribani miaka 8 sasa hivyo ameishukuru serikali kwa kuamua kukutana nao ili kutatua suala la mafao.

Hata hivyo Wizara hiyo imepanga kufanya zoezi la kusikiliza malalamiko ya Wastaafu nchi nzima ikiwa ni Utekelezaji wa  agizo la rais Samia Suluhu Hassan aliloliagiza siku ya wafanyakazi Duniani( Mei mosi) iliyofanyika kitaifa mwaka huu Jijini Dodoma mwezi may.

Comments