YUHOMA EDUCATIONAL LTD YASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU YA JUU DAR, MKURUGENZI WAKE ATOA USHAURI KWA WANAOTAKA KUSOMA NJE YA NCHI
YUHOMA EDUCATIONAL LTD YASHIRIKI MAONYESHO YA ELIMU YA JUU DAR, MKURUGENZI WAKE ATOA USHAURI KWA WANAOTAKA KUSOMA NJE YA NCHI
![]() |
![]() |
Mkazi wa jiji la Dar es salaam akifuatilia Kwa makini maelezo ya Moja ya watumishi wa Taasisi ya Yuhoma Educational LTD katika Banda la Taasisi hiyo inayoshiriki Katika maonesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja.![]() |
![]() |
| Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia Kwa makini maelezo ya Moja ya watumishi wa Taasisi ya Yuhoma Educational LTD katika Banda la Taasisi hiyo inayoshiriki Katika maonesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja. |

Na Thadei PrayGod,
Dar es salaam.
Taasisi ya elimu inayojihusisha na utoaji wa ushauri wa kielimu Kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nje ya nchi pamoja na kuwatafutia wanafunzi hao vyuo vikuu nje ya nchi,Yuhoma Educational limited inashiriki kwenye maonyesho ya 17 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika Katika Viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na tume ya vyuo vikuu TCU.
Akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Banda la Taasisi hiyo Mkurugenzi mkaazi wa Yuhoma Educational LTD, Yusuph Yahaya amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikitoa ushauri kwa wanafunzi juu ya kozi za kusomea ili kuendana na soko la ajira la dunia pamoja na kuwapeleka wanafunzi hao kusoma katika vyuo mbalimbali duniani vinavyotoa elimu bora na yenye kuwajenga vijana kitaaluma.
Amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakipata shida katika uchaguzi wa vyuo ambavyo wanataka kusoma na aina ya kozi ambazo wanataka kusomea jambo ambalo Taasisi hiyo imetoa suluhusho Kwa wanafunzi hao Kwa kuhakikisha wanapata ushauri elekezi juu ya kile wanachotaka kusomea hasa katika vyuo vilivyopo nje ya nchi pamoja na kuutumia Taasisi hiyo kama wakala wa kuwatafutia vyuo bora nje ya nchi.
Hata hivyo amewataka vijana hapa nchini kujiendeleza kielimu Ili waweze kupambana na soko la ajira la dunia kwani nchi nyingi za kiafrika wageni hupata ajira na kufanya wenyeji kutokuwa na ajira kutokana na kukosa elimu stahiki inayoendana na soko la ajira.
Akizungumzia changamoto ya baadhi ya wazazi ambao wanataka watoto wao waende kusoma nje ya nchi Bw Yahaya amesema kuwa bado Kuna uelewa mdogo tangu kutokea Kwa janga la covid 19 pamoja na vita nchini Ukraine Kwa wazazi kutokujua kuwa tayari anga la kimataifa limeshafunguka na wanaweza kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi.
Pia ameiomba serikali kuwakutanisha na balozi za nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini pamoja Taasisi hiyo ya Yuhoma kwani kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa visa Kwa wakati Kwa wanafunzi wanaoenda kusoma nje ya nchi jambo ambalo limekuwa Kwa kiasi Fulani likikwamisha juhudi za Taasisi hiyo yenye Nia njema na watanzania katika kuhakikisha wanapata vyuo bora nje ya nchi vitakavyozalisha wataalamu katika nyanja mbalimbali.
Amesema elimu ndio njia pekee ambayo vijana wakiwemo watanzania wanaweza kuitumia kupata ajira za uhakika na zenye maslahi makubwa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mbali na hayo pia ameiomba Serikali iwaamini na kuwasaidia vijana wenye ndoto za kwenda kusoma nje ya nchi pia wawawezeshe mikopo waweze kufikia malengo yao.
Yuhoma Educational ltd ni Taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu nje ya nchi ambao watanzania wengi wameisha nufaika na taasisi hiyo.
Hata hivyo katika hatua nyingine mkurugenzi huyo ameipongeza serikali kupitia tume ya vyuo vikuu TCU Kwa kuandaa maonyesho hayo ambayo huwakutanisha mawakala wa vyuo,vyuo vikuu na wanafunzi huku akiwataka vijana wanaotaka kusoma vyuo vya nje ya nchi kutembelea Banda la Taasisi hiyo ili kupata ushauri juu ya kozi ambazo wanataka kusomea pamoja na kushauriwa na kuuunganishwa Moja Kwa moja na vyuo hivyo vikubwa duniani.






Comments