AZAM TV WASHUSHA BEI YA KISIMBUZI CHA ANTENA KUANZIA SEPTEMBA 1.
AZAM TV WASHUSHA BEI YA KISIMBUZI CHA ANTENA KUANZIA SEPTEMBA 1.
Afisa mwendeshaji mkuu,AzamTv Ltd,Loth Mziray Akizungumza wakati kampuni hiyo ikitangaza kushusha bei ya kisimbuzi chake cha antena kuanzia kesho. |
Na Thadei PrayGod
Dar es salaam.
Kampuni ya Azam Tv LTD leo imetangaza rasmi mwendelezo wa promosheni yake ya ‘Mzigo siyo UTANI’ wenye kauli ‘Mzigo umeshuka bei’ ambapo bei ya kisimbuzi chake Cha antena itashuka rasmi nchini kote kuanzia kesho September 1,2022
Akizungumza wakati akitangaza kushuka Kwa bei ya kisimbuzi hicho wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za biashara na masoko za kampuni hiyo zilizopo masaki Jijini Dar es salaam, Afisa mwendeshaji mkuu wa Azam Tv Ld Loth Mziray amesema kuwa wameamua kushusha bei ili huduma za matangazo ya televsheni ziwafikie wananchi (wateja)wengi zaidi.
Amesema kuwa kuanzia kesho septemba 1,2022 kisimbuzi hicho kitauzwa Kwa shilingi 79,000 kikiwa na antena yake ambapo awali kiliuzwa Kwa shilingi 99,000 huku kisimbuzi hicho kiliuzwa Kwa shilingi 59,000 bila antena ambapo awali kiliuzwa Kwa shilingi 85,000.
“ndugu waandishi wa habari sisi kama Azam tv tumekuwa na nia madhubuti ya kuwafikia wananchi wote,mijini na vijijini,ndani na nje ya nchi,na kuhakikisha tumejiimarisha kuwapa maudhui bora,bidhaa bora za kisasa,kwenye huduma zetu zote ili kusambaza burudani kwa wote kwa bei nafuu zaidi”aliongeza mwendeshaji huyo mkuu wa Azam tv.
Aidha ameongeza kuwa kampuni hiyo pia itapeleka bidhaa zake za antena Kwa mara ya kwanza katika mikoa mipya 6 ambayo awali haikuwa ikipata huduma hizo za kisimbuzi cha antena na kufanya jumla ya mikoa kufikia 17 mpaka sasa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu.
Akiitaja mikoa hiyo ambayo itaanza kufaidi huduma ya kisimbuzi cha antena zinazotumia mfumo wa DTT amesema kuwa pamoja na Kigoma mjini,Tabora,Lindi mjini, Njombe (Makambako), Kigoma, pamoja na wilaya za Tunduru na Sumbawanga mjini.
Lengo lingine la kushusha bei ya kisimbuzi na pia kutanua wigo wa huduma zake katika mikoa mingine 9 ni kurahisisha huduma kuwafikia watanzania wengi Kwa wakati na bei rafiki ambayo yeyote anaweza kuimudu.
Naye meneja mauzo na usambazaji wa kampuni hiyo Adam Ndimbo amesema kuwa mauzo ya visimbusi hivyo yataanza na shamrashamra katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na wilaya zake zote kuanzia kesho ambapo watapita mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
“Hakuna sababu ya Mtanzania yoyote hivi sasa kukosa kisimbuzi cha antena cha AzamTV,hivyo tunaahidi kuendelea kuwapa burudani watanzania alisema Meneja huyo wa Mauzo na Usambazaji Azam TV
Meneja mauzo na usambazaji,AzamTv Ltd,Adam Ndimbo Akizungumza wakati kampuni hiyo ikitangaza kushusha bei ya kisimbuzi chake cha antena kuanzia kesho. |
Visimbuzi hivyo vya antena vya Azam Tv vitaanza kuuzwa kwa bei ya punguzo kote nchini kuanzia kesho.
Comments