COSTECH YAWAJENGEA UWEZO MAMENEJA WA USIMAMIZI WA UTAFITI NCHINI

 

COSTECH YAWAJENGEA UWEZO MAMENEJA WA USIMAMIZI WA UTAFITI NCHINI

.............................

Arusha – COSTECH

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji Tafiti (DRCP) imeendesha warsha ya siku 3 kuanzia tarehe 29 - 31 Agosti 2022, ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ili kuwajengea uwezo mameneja usimamizi miradi ya tafiti kwa Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleo nchini - Jijini Arusha.

“ Naipongeza Tume kwa mafunzo ya uandaaji miradi shindani , binafsi nimefurahishwa na program hii pamoja na washiriki waliojitokeza, kubwa zaidi niipongeze COSTECH kwa juhudi inazozichukua kujenga uwezo kwa watafiti ili kuandaa watafiti waliobora kwa Tanzania ya kesho” Alisema Prof. Hosya.

Prof Hosya ambae ni mkufunzi alifafanua, ni muhimu washiriki kuzingatia maarifa na ujuzi waliopatiwa ikiwemo taratibu za manunuzi , utawala bora na upembuzi yakinifu( _due diligence_) ya miradi ili kuongeza tija ya undeshaji miradi ya kitafiti nchini.

Kwa upande wake, Dkt Godsteven Maro toka Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kwa niaba ya mameneja wenzake aliipongeza COSTECH kwa kuandaa warsha hiyo.

" Nyuso za washiriki wote ni zenye furaha na changamfu , tunaishukuru sana COSTECH kwa kuratibu warsha hii na wawezeshaji kwa kutupatia mafunzo mazuri" alisema Dkt Maro

Kwa upande wake, Bi Rose Mosha aliishukuru Tume kuendelea kufadhali mafunzo hayo kwa mara nyingine tena.

Akihitimisha mafunzo hayo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Meneja Sayansi ya Jamii Mha. Mashuhuri Mushi alitoa rai kwa washiriki kuzingatia mafunzo waliyoyapata ili kutumia maarifa na elimu waliyojengewa kwa wale ambao hawakuweza kufika hapa ili wananchi waweze kunufaika na maarifa hayo.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu amenituma niwape ahadi watafiti COSTECH itaendelea kushirikiana na Taasisi zenu kupitia utaoji mafunzo kadri itakavyofaa kulinganana na mamlaka iliyokasimiwa chini ya Sheria na 7 ya mwaka 1986" alisema Mha. Mashuhuri.

Comments