NSSF Yasema Iko vizuri kuhudumia wanachama wake yapanga Kukusanya Trioni 7.3 Mwaka wa Fedha 2022/ 2023.

 NSSF Yasema Iko vizuri kuhudumia wanachama wake yapanga Kukusanya Trioni 7.3 Mwaka wa Fedha 2022/ 2023.




Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imepanga kukusanya kiasi Cha shilingi trioni 7.3 katika Mwaka wa fedha 2022 / 2023,ambapo fedha hiyo inatokana na michango ya wanachama wa mfuko huo.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw.Masha Mshomba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya NSSF kwa Mwaka wa fedha 2021/ 2022,ambapo amesema kwamba Mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni  2022, NSSF imefanikiwa kukusanya shilingi trioni 6.2. kiasi ambacho kimeimarisha maradufu utoaji wa huduma kwa wanachama.

Bw.Mshombe amesema kwamba kwa Mwaka huu wa fedha 2022/2023 NSSF imejiwekea vipaumbele kabambe ili kuufanya Mfuko huo kuendelea kuimarika zaidi ikiwemo kuongeza wanachama kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi,kuboresha njia za kukusanya na kuwasilisha michango kwa njia yakieletroniki(TEHAMA),kuboresha huduma kwa wanachama,kufanya uwekezaji salama nakuepuka upotevu wa fedha ili kuweza kulipa mafao kwa wanachama.

Amesema kwamba NSSF inaendelea na ukamilishaji wa miradi yake ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo la biashara lililopo mkoani Mwanza,pamoja na jengo lililopo Mtaa wa Mzizima,Mradi wa Nyumba za Kupangisha  na kuuza huko eneo la Dungu Kigamboni,Tuangoma na Kijichi Wilayani Temeke ,pamoja na kiwanda cha Sukari kinachojengwa Mkoani Morogoro ambacho kinatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2022/2023.

Aidha pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF amesema Kwamba wanaendelea na uimarishaji wa usimamizi wa Mapato ili kuahakikisha fedha hizo zinatumika kwa matumizi stahiki ili kuleta ustahimilivu wa mfuko,ambapo mfuko huo unatakiwa kutumia asilimia 10 pekee ya mapato yanayokusanywa na mfuko huo.

Comments