NSSF YAFADHILI SH M. 500 UTENGENEZWAJI WA KAZIDATA YA DIASPORA
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu akimsikiliza
zinazongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Diaspora wanachangia kikamilifu na kuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa taifa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii NSSF Umeweka wazi kuwa Diaspora ni kundi muhimu katika uwekezaji nchini.
Hayo yameelezwa leo Agosti 26,2022 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uthaminishaji , Takwimu na Usimamizi wa habari na mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ibrahim Zakaria Maftah wakati wa hafla fupi ya utiaji saini hati ya Makubaliano ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na NSSF kwa ajili ya kupokea ufadhili wao katika matengenezo ya Mfumo wa kutunza taarifa za Diaspora Kidigitali .
Ibrahim Maftah amesema mfumo huo utatoa uratibu wa kazi mbalimbali za Diaspora kufanyika kwa mtandao kitendo kitakachopelekea kutoa fursa kwa NSSF kutangaza fursa za miradi mbalimbali ya uwekezaji zitolewazo na mfuko
“Kitendo cha NSSF kusaini makubaliano hayo kinaonesha utayari na muelekeo wetu katika kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika eneo la Diaspora,” alisema Bw. Maftah.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana amesema kupitia makubaliano walioingia na NSSF wanaimani
kuwa kupitia mfumo huo kutawezesha kuwasajili na kuwatambua Diaspora Watanzania waliopo katika mataifa mbalimbali ulimwenguni na kuwawezsha kupata huduma za kimaendeleo , biashara , uchumi na uwekezaji hapa nchini .
“Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ambayo yataiwezesha NSSF kutoa Shilingi Milioni 50 ambazo zitaiwezesha Wizara kutengeneza Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, kitendo hiki ni mwanzo wa ushirikiano wa muda mrefu ambao Wizara umekuwa nao na NSSF, ni matarajio ya Wizara kuwa NSSF itahuisha program yao ya Diaspora na kubuni programu mpya ili kutoa huduma kwa Diaspora wetu na wao kunufaika zaidi na programu hizo,” alisema Balozi Bwana.
Comments