PSPTB yasisitiza kuwa ni lazima Maafisa Ununuzi na Ugavi Kujisajili Kwenye Mfumo Mpya

 PSPTB yasisitiza kuwa ni lazima Maafisa Ununuzi na Ugavi Kujisajili Kwenye Mfumo Mpya


 

https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif

https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi PSPTB) Godfred Mbanyi amewataka wataalamu wa ununuzi wa mashirika na taasisi  zote za serikali na binafsi kuhakikisha wanajisajili kwenye bodi hiyo kwani serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imeandaa mfumo mpya wa manunuzi ambao bila kujisajili hawawezi  kuingia katika mfumo huo.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amebainisha kwamba  ili kudhibiti manunuzi yasiyo na ubora serikali imeamua kuanzisha mfumo mpya ambao kila afisa manunuzi na ugavi anapaswa kujisajili ili aweze kutambulika haraka anapobainika kukiuka taratibu za ununuzi.

Aidha Mbanyi amesema kwamba mfumo huo mpya unaoandaliwa na serikali nakusimamiwa na  bodi hiyo utaruhusu maafisa ununuzi na ugavi waliosomea taaluma hiyo na kusajiliwa na PSPTB ndio pekee watakoingia kwenye mfumo huo  wa manunuzi nakuwezesha kuwachukulia hatua wale wanaoshindwa kufuata taratibu za taaluma hiyo.

“ Tunamatumaini makubwa kuwa huu mfumo utasaidia kuondoa malalamiko yakuwepo kwa manunuzi yanayokiuka sheria za ununuzi na ugavi nakupelekea serikali na skta binafsi kupata hasara,hivyo bodi inawataka maafisa manunuzi wote kuhakikisha wanajisajili katika mfumo huo haraka iwezekanavyo ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza” amesema Mbanyi.

Hali kadhalika  Mkurugenzi Mtendaji huyo w PSPTB  amesisitiza kuwa hivi karibuni wataanza oparesheni maalumu yakukagua mashirika ya umma na binafsi kama yamesajiri wataalamu waliosomea taaluma ya manunuzi na ugavi pamoja na kusajiliwa na bodi hiyo.

Hata hivyo amefafanua kuwa ukaguzi huo utaanza kwa mashirika na taasisi kubwa za serikali na  binafsi  ikiwa lengo ni kuhakikisha wanawabaini wale wataalamu wa manunuzi na ugavi wasio na sifa na pia kuona kama hawajasajiliwa na bodi ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Comments