SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW LAELEZA MIPANGO YAKE KUWAINUA WATOTO WA KITANZANIA KIELIMU
SHIRIKA LA THE FOUNDATION FOR TOMORROW LAELEZA MIPANGO YAKE KUWAINUA WATOTO WA KITANZANIA KIELIMU.

![]() |
| Meneja wa program ya mafunzo kwa walimu wa shirika la The Foundation for Tomorrow,Noah Kayanda wa kwanza kushoto akizungumza na baadhi ya wadau waliotembelea Banda la shirika hilo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere JNICC jijini Dar es salaam. Na mwandishi wetu, Dar es salaam |
Shirika la lisilo la kiserikali la The Foundation for Tomorrow linashiriki katika maonyesho kando ya mkutano wa kimataifa wa masuala ya elimu bora ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania Ten/met
Akizungumza na waandishi wa habari Mbale ya banda la shirika hilo,mkurugenzi wa shirika hilo la kimataifa lisilo la serikali, Thabisani Ncube amesema kuwa shirika limekuwa likitoa msaada katika masuala ya elimu kwa kuwawezesha kupata elimu watoto wanaotoka katika mazingira magumu
Na wamekuwa na programme mbalimbali ikiwemo ya ufadhili wa masomo ambapo limekuwa likiwasapoti wanafunzi kwa kuwalipia ada na mahitaji mengine ya shule kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita ili waweze kufikia malengo yao ya kimaisha na kielimu.
“shirika letu limeona elimu ndiyo msingi wa maendeleo na kwa maana hiyo sisi tumekuwa tukitoa scholarship ya masomo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambayo yanawafanya washindwe kupata elimu bora hivyo tunawasaidia kwa kuwasomesha”aliongeza Bw Thabisani Ncube.
Ameongeza kuwa shirika hilo lenye miaka 15 mpaka hivi sasa tangu lianze shughuli zake na lenye makao yake jijini Arusha na kwa mwaka huu wameanza kujenga maeneo ya kijamii ya kujifunzia ambayo yatawawezesha wananchi kujifunza kusoma na kuandika ndani na nje ya jiji hilo na wameanza katika eneo la Usa river ili kuwasaidia wanafunzi wa kitanzania kuendana pia na kasi ya ukuaji wa kidigitali ili kusaidia katika maendeleo ya Taifa.
Hata hivyo amesema kuwa katika vituo hivyo vya kijamii vya kujifunzia pia watatoa mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara kwa kuwa wanaamini kama WATU wengi watakuwa na mawazo bora ya kibiashara na kuamini kuwa zitawainua kiuchumi wanapaswa kufundishwa jinsi ya kuziendesha.
Aidha akiuzungumzia programe ya walimu mkurugenzi huyo amesema kuwa shirika limekuwa likitoa mafunzo kwa walimu walioko kazini ili kuwajengea uwezo katika kuhakikisha wanawapa watoto wa kitanzania elimu bora inayoendana na mazingira ya kitaaluma iliyo bora katika maislha.
Kwa upande wake meneja program ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda amesema kuwa pia shirika la The FOUNDATION for Tomorrow limekuwa likitoa mafunzo kwa viongozi wa shule katika ngazi mbalimbali ili kuhakikisha kubwa shule zao zinatoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania na hatimaye kujenga Taifa bora lenye misingi madhubuti ya elimu.
Aug 18 2022
Published by
SisiNihabari



Comments