SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LASEMA LINATHAMINI MCHANGO WA VIJANA: KUELEKEA TUZO ZA TEYA 2022
SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LASEMA LINATHAMINI MCHANGO WA VIJANA: KUELEKEA TUZO ZA TEYA 2022
meneja kampeni na utetezi shirika la Save the Children Jovitha Mlay akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)kando ya ukumbi wa maktaba mpya,chuo kikuu cha Dar es Salaam kulikofanyika uzinduzi wa tuzo za vijana chipukizi kwa mwaka 2022. |
Dar es Salaam.
Shirika la Save the Children limesema linathamini mchango wa vijana katika maendeleo ya Taifa ndio maana limeamua kushirikiana na shirika la African Youth Transformation AYT katika kuandaa tuzo za vijana chipukizi TEYA 2022
Akizungumza kando ya mkutano wa uzinduzi wa tuzo hizo kwa mwaka huu ulioenda sambamba na maonyesho ya vijana na mashirika mbalimbali katika ukumbi wa maktaba mpya ya chuo kikuu cha Dar es salaam meneja kampeni na utetezi shirika la Save the Children Jovitha Mlay amesema wameamua kushirikiana na AYT katika kuandaa tuzo hizo za vijana chipukizi TEYA 2022 na kuanzisha kipengele cha Youth innovation challenge ambapo lengo lake ni kutambua mchango wa vijana Katika kukuza uchumi kupitia makundi mbalimbali ikiwemo,
Mabadiliko ya tabia ya nchi na ‘green business’,Ulinzi wa watoto,Afya ya uzazi pamoja na teknolojia
“katika tuzo hizi ambazo mchakato wake unaendelea leo sisi kama save the children kazi yetu kubwa ni kufanya kazi na watu,tunafanya kazi katika kutetea haki na maslahi ya watoto na tunaangalia maeneo matatu ambayo ni haki ya mtoto kuishi,kujifunza,kushiriki pamoja na kulindwa na tunatambua nafasi yetu ya kimkakati katika kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea kukua mpaka kuwa vijana na hatimaye WATU wazima”alisema meneja huyo wa kampeni na utetezi wa Save the children.
Amesema wao kama viungo kati ya watoto na vijana na kulingana na sera ya Tanzania ambayo inamtafsiri kijana kama mtu anayeanzia miaka 15 na 35 hivyo wameamua kushiriki katika tuzo hizo za Vijana TEYA 2022 ili kuwezesha vijana kuonyesha mchango wao,vipaji walivyo navyo pamoja na mikakati waliyojiwekea kama vijana.
Hata hivyo ameongeza wao kama Save The Children wanaamini kama vijana watajengewa mazingira wezeshi,kisera,kimkakati,kirasilimali,mafunzo pamoja na taarifa wanaweza kufanya mambo ambayo yatakuza uchumi wa nchi.
“shirika la save the children katika mpango mkakati wake linafanya kazi na serikali moja kwa moja na hii ni kuwezesha mifumo ya serikali kufanya kazi,kujenga uwezo,kuimarisha miundombinu pamoja na kufanya tafiti tukishirikiana pia na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali kama Africa Youth Transformation katika kuwapatia vijana rasilimali ili waweze kutekeleza mipango waliyojiwekea”aliongeza Bi Jovitha Mlay
Comments