TAMASHA LA TWENZETU KWA YESU 2022 KUTIKISA DAR,JUMAMOSI HII
TAMASHA LA TWENZETU KWA YESU 2022 KUTIKISA DAR,JUMAMOSI HII.
Dar es salaam.
Lile tamasha kubwa la vijana hapa nchini linalohusisha pia muziki wa injili linaloshirikisha vijana mbalimbali nchi nzima linatarajiwa kufanyika agosti 13,mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,mkurugenzi mtendaji wa upendo media Neng'da Johannes ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amesema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mahiri wa muziki wa injili ndani na nje ya nchi.
Aidha amesema tamasha hilo limekuwa pia likitoa elimu kwa vijana juu ya suala la maadili mema kwa vijana na limekuwa ni mwanga mkubwa kwa vijana hapa nchini na makanisa ya kilutheri barani Africa.
Akiwataja wasanii watakaotumbuiza tamasha hilo mkurugenzi huyo amesema kuwa ni pamoja na,
Zaza Moketi kutoka south Afrika
Rose Muhando
Rehema Simfukwe
AIC Chang’ombe
Essence of worship na wengineo.
Aidha amesema kuwa suala la ulinzi kwa siku ya tamasha litakuwa ni la uhakika huku akiwataka vijana wenye magari yao kutoyaacha wakihofia usalama kwani jeshi la polisi Temeke limeahidi kutoa ushirikiano madhubuti huku akiwataka wazazi kuwapeleka watoto wao siku ya tamasha.
Naye meneja wa uwanja wa Uhuru,Redempta Nyahonge amesema wao kwa upande wa uwanja wamejiandaa vizuri siku ya tamasha hilo ambapo askari polisi zaidi ya 150 watakuwepo na watafungua mageti yote manne makubwa ili kuwawezesha wahudhuriaji wa tamasha hilo kuingia uwanjani kwa utulivu na amani.
Tamasha la Twenzetu kwa yesu 2022 “twenzetuConcert” linatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya AGOST 13,2022 kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
Comments