TUZO ZA VIJANA CHIPUKIZI 2022,SERIKALI YASEMA INAIPITIA SERA YA VIJANA.

 

TUZO ZA VIJANA CHIPUKIZI 2022,SERIKALI YASEMA INAIPITIA SERA YA VIJANA.

Serikali imesema inaifanyia mapitio sera ya vijana ya mwaka 2007 ili kuja na sera bora na imara zaidi kwa vijana.


Akizungumza wakati akizindua tuzo za vijana chipukizi mwaka 2020 na mdahalo wa siku mbili wa vijana ulioandaliwa na taasisi  ya African Youth Transformation AYT,waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu, Profesa Joyce NDALICHAKO amesema mara baada ya serikali kuifanyia mapitio sera hiyo kwa kuwashirikisha vijana itakuja na suluhisho bora kwa kuhakikisha vyombo vya kuwasimamia vijana ikiwemo baraza la vijana vinaanzishwa vikiwa madhubuti.


amesema serikali inafurahia uwepo wa hazina ya vijana wenye ubunifu hapa nchini na utawaunga mkono katika kila hali.

Aidha ameipongeza taasisi ya AYT kuandaa mdahalo maalum kwa vijana kujadili maswala mbalimbali pamoja na maonyesho ya kiteknolojia ya vijana yanayofanyika katika maktaba mpya ya chuo kikuu cha Dar es salaam Kwa siku mbili.

Ameongeza kuwa serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kuongeza ajira kwa watanzania hapa nchini wakiwemo vijana wa kitanzania.


Amesema serikali kupitia wizara yake inaendelea na mpango wake wa mafunzo kwa vijana katika sekta mbalimba za uanagenzi kwa vijana na imetenga bilioni 90 kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo sambamba na kuendesha mafunzo ya uzoefu kazini ambapo tayari vijana zaidi ya 2000 wamepata mafunzo hayo.


Aidha amewataka vijana wanaochukua mikopo katika mfuko wa maendeleo kwa vijana na ule wa asilimia 10 ya halmashauri mbalimbali nchini kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili vijana wengine waweze kunufaika nayo.


“kama serikali mikopo huu tumeiwekea muda mrefu wa kuirudisha mpaka miezi 24 na kuongeza kiwango cha kukopa kupitia mfuko wa maendeleo kwa vijana kutoka milioni 10 hadi 50 kwa wakati mmoja hivyo nawasihi vijana kuchangamkia fursa hizi ya mikopo na wairejeshe kwa wakati ili na wengine wakopesheke”alisema Waziri, Prof Ndalichako

Naye meneja kampeni na utetezi wa taasisi ya Save the Children Jovitha Mlay amesema wameamua kushirikiana na AYT katika kuandaa tuzo hizo za vijana chipukizi TEYA 2022 na kuanzisha kipengele cha Youth innovation challenge ambapo lengo lake ni kutambua mchango wa vijana Katika kukuza uchumi kupitia makundi mbalimbali ikiwemo,

Mabadiliko ya tabia ya nchi na ‘green business’,Ulinzi wa watoto,Afya ya uzazi pamoja na teknolojia


katika tuzo hizi ambazo mchakato wake unaendelea leo sisi kama save the children kazi yetu kubwa ni kufanya kazi na watu,tunafanya kazi katika kutetea haki na maslahi ya watoto na tunaangalia maeneo matatu ambayo ni haki ya mtoto kuishi,kujifunza,kushiriki pamoja na kulindwa na tunatambua nafasi yetu ya kimkakati katika kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea kukua mpaka kuwa vijana na hatimaye WATU wazima”alisema meneja huyo wa kampeni na utetezi wa Save the children.

Amesema wao kama viungo kati ya watoto na vijana na kulingana na sera ya Tanzania ambayo inamtafsiri kijana kama mtu anayeanzia miaka 15 na 35 hivyo wameamua kushiriki katika tuzo hizo za Vijana TEYA 2022 ili kuwezesha vijana kuonyesha mchango wao,vipaji walivyo navyo pamoja na mikakati waliyojiwekea kama vijana.

Hata hivyo ameongeza wao kama Save The Children wanaamini kama vijana watajengewa mazingira wezeshi,kisera,kimkakati,kirasilimali,mafunzo pamoja na taarifa wanaweza kufanya mambo ambayo yatakuza uchumi wa nchi.

“shirika la save the children katika mpango mkakati wake linafanya kazi na serikali moja kwa moja na hii ni kuwezesha mifumo ya serikali kufanya kazi,kujenga uwezo,kuimarisha miundombinu pamoja na kufanya tafiti tukishirikiana pia na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali kama Africa Youth Transformation katika kuwapatia vijana rasilimali ili waweze kutekeleza mipango waliyojiwekea”aliongeza Bi Jovitha Mlay

Mkurugenzi mkuu wa taasisi Youth Transformation AYT ,Justine Mponda amesema taasisi hiyo kuandaa mdahalo huo pamoja na Tuzo za vijana chipukizi pia imekuwa na programme mbalimbali ikiwemo ya youth baraza ambayo huwakutanisha vijana katika midahalo mbalimbali inayokuja na maoni ambayo yatachangia utekelezaji wa shughuli za taasisi na serikali kwa ujumla.

“kama taasisi tunaamini katika kuwawezesha vijana wa Tanzania katika masuala mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya jamii na ndiyo maana tunawaunga mkono katika nyanja mbalimbali.”alisema mkurugenzi huyo

Aidha ameiomba serikali ya Tanzania kuendelea kuandaa vyema mpango wa kuwasikiliza, kuwasaidia na kuwawezesha vijana kwa kutenga chombo maalum cha kuwasaidia vijana hao pasipo mipaka ya kisiasa na kiitikadi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Naye mkuu wa wilaya ya Ubungo,Herry James amepongeza hatua ya AYT kuandaa mdahalo huo ambao utaenda sambamba na tuzo na kuongeza kuwa serikali itaendelea kuthamini mchango wa vijana katika kukuza  katika nyanja mbalimbali.

Amesema kuwa yeye kama kijana aliyeaminiwa na Rais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwasaidia vijana kwani ni takwa la kiserikali huku akiwataka vijana wa wilaya hiyo kuendelea kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi ili serikali iandae mkakati madhubuti wa kuwasaidia.


Mratibu wa tuzo hizo  amesema wataendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya sita katika kuwainua vijana wa kitanzania sambamba na kuhakikisha wanazijua fursa mbalimbali za kiteknolojia.


Amepongeza shughuli ya sensa ambayo inaendelea kote nchini na kuwataka vijana ambao bado hawajafikiwa na makarani wa sensa kutoa ushirikiano ili serikali iandae mkakati madhubuti wa namna ya kuwasaidia wananchi wake baada ya kujua idadi yao kamili


Comments