DKT INTERNATIONAL TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA UZAZI WA MPANGO DUNIANI, YATOA ZAWADI KWA WAZAZI HOSPITALI YA MBAGALA RANGITAT


 DKT INTERNATIONAL TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA UZAZI WA MPANGO DUNIANI, YATOA ZAWADI KWA WAZAZI HOSPITALI YA MBAGALA RANGITATU. 


Na Thadei PrayGod

Ili Taifa lolote liendelee kiuchumi na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu maishani ni lazima Taifa hilo lihimize wananchi wake kupanga katika malezi ya watoto wao hasa kuhamasisha katika suala la uzazi wa mpango. 


Kwa kutambua hilo hii leo Dkt International Tanzania Kwa kushirikiana na hospitali ya Mbagala,Rangitatu leo wameungana na ulimwengu katika kuadhimishaa siku ya Uzazi wa mpango inayoadhimishwa dunuani kote Septemba 26 kila mwaka.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika hospitali hiyo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema kuwa siku ya Uzazi wa mpango ni siku muhimu ambayo huwakumbusha wananchi kuzimgatia na kutumia uzazi wa mpango wanapopanga jinsi gani ya kupata,kulea na KUHUDUMIA watoto wao hivyo akawasitiza wananchi kutumia uzazi wa mpango katika kujenga familia zao.

Katika maadhimisho hayo Dkt International Tanzania pia leo imezindua kampeni yake inayojulikana kama 'Jipange' ambayo inahamashisha wananchi kutumia vidonge vya uzazi wa mpango Trust Liliy vya muda mrefu, Trust Daisy vya muda mfupi, Kitanzi na Fiesta Condomu na Bull Condomu.

 

DC amewaambia wahudhuriaji wa maadhimisho hayo kuwa ili kujenga familia bora ni lazima wazazi wawe mipango thabiti na mikakati mizuri juu ya suala la uzazi Kwa kuhakikisha wanatumia njia sahihi za uzazi wa mpango zinazoshauriwa na wataalamu wa afya ya uzazi.

“Familia zetu tunatakiwa kujipanga katika swala zima la uzazi kwani litasaidia katika maendeo yetu na ya taifa kwa kuwa tukifanikiwa kupata watoto kwa mpango itatusaidia katika malezi bora ambayo itatusaidia kupunguza ‘Panya Road’ na watoto wa mitaani,” amesema Mwegelo.

Hata hivyo katika hatua ya kufurahisha,  Mkuu huyo wa wilaya ametembelea Wodi za mama waliotoka kujifungua na kuwapatia zawadi kutoka DKT Internationl Tanzania, huku akiipongeza kampuni hiyo kwa kuamua kuanzia katika wilaya ya Temeke kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kufundisha njia sahihi za kutumia pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uzazi wa Mpango katika hospitali ya Mbagala, Elizabeth Bita, ameeleza kuwa kwa mwezi ofisi yake inapokea watu zaidi ya 700 wanaofata uzazi wa mpango na wengi wao hupenda njia ya kitanzi cha miaka mitatu kwa kuwa ni kirahisi.

Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Daktari Irene Haule amewaomba kampuni ya DKT Internationl Tanzania, kutembea mashuleni ili kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kuwa wanafunzi wengi wanakatisha masomo kwa sababu ya kupata mimba zisizotarajiwa.


Naye meneja masoko  wa kampuni ya Dkt Tanzania, Deogratius Kithama, alishukuru mkuu wa wilaya kwa kuungana nao katika uzinduzi wa kampeni ya Jipange na kuahidi kutoa ushirikiano pale watakapo hitajika katika upande wa uzazi wa mpango ili kutengeneza jamii bora.

Ameongeza kuwa wao kama Dkt International Tanzania wataendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango huku akisisitiza kuwa kampeni yake ya 'jipange' itakuja na majawabu lukuki juu ya umuhimu wa wananchi kutumia uzazi wa mpango kupitia vidonge vinavyosambazwa na kampuni hiyo. 

Comments