KAMPUNI YA REJAA REAL ESTATE YAMTAMBULISHA MUIGIZAJI SIWA KIKALA KAMA BALOZI WAKE.

 KAMPUNI YA REJAA REAL ESTATE YAMTAMBULISHA MUIGIZAJI SIWA KIKALA KAMA BALOZI WAKE. 



Dar es salaam. 

Kampuni inayojihusisha na masuala ya uuzaji wa viwanja na mashamba ya Rejaa Real Estate leo imemtangaza muigizaji Siwa Kikala ‘SiwaKombolela’ kama balozi wa kampuni hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam wakati wa utambulisho wa balozi huyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Revocatus  amesema kama kampuni wamevutiwa na kazi za msanii huyo katika jamii hivyo wakaona ni vyema awe balozi wa kampuni.


Amesema kampuni hiyo itaendelea kuuza viwanja na mashamba Kwa watanzania Kwa bei nafuu bila longolongo huku akiwataka watanzania kuwa na utaratibu wa kununua viwanja.


“Si kama Rejaa Real estate hatuna longo longo katika uuzaji wa viwanja na mashamba na nawaomba watanzania wanunue viwanja na mashamba kupitia sisi na hata huyu balozi wetu tumejiridhisha na balozi wetu kupitia tamthilia ya kombolela nadhan wote mnamjua ushawishi wake ndiyo maana tumempa mkataba” aliongeza Mkurugenzi huyo.


Amewataka wakazi wa Jiji la Dar es salaam ambao wana ndoto za kumiliki viwanja vyao kutembelea ofisi za kampuni hiyo zilizopo Makumbusho, Kijitonyama. 


Aidha Kwa upande wake mwigizaji Siwa Kikala ameishukuru kampuni ya Rejaa Real estate Kwa kuamua kumpa ubalozi huo na kuahidi kuwa atafanya kazi katika kuhamasisha watanzania kujinunulia viwanja Kwa ajili ya makazi na mambo mengine kumpitia kampuni hiyo.


Ameongeza kuwa kampuni hiyo Kwa sasa Ina miradi mbalimbali ikiwemo katika eneo la kigamboni ambapo Kuna viwanja vinavyopatikana Kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania ataweza kuimudu.


Hata hivyo amewataka wasanii wenzake Kuanza utaratibu wa kujenga nyumba zao wenyewe na kuachana na kupanga ili baadaye wasije kuhangaika pa kukaa Kwa kuchezea hela zao kula bata badala ya kuwekeza katika ujenzi. 


Kwa upande wake msimamizi wa miradi wa kampuni hiyo,Mohammed Rashid amesema kuwa kampuni hiyo Ina miradi katika maeneo ya Bagamoyo, Mbopo, Madale, Bagamoyo Mjini, Mlandizi, Goba na mnunuaji anaweza kulipa kidogokidogo kuanzia shilingi laki Moja kila mwezi mpaka pale atakapokamilisha malipo yake na kupata hati. 


Comments