MASHINDANO YA SARPCO YATAMATIKA,IGP WAMBURA ASEMA YAMECHOCHEA USHIRIKIANO.

 MASHINDANO YA SARPCO YATAMATIKA,IGP WAMBURA ASEMA YAMECHOCHEA USHIRIKIANO.

Na Thadei PrayGod

Dar es salaam.

Mashindano ya majeshi ya polisi wa nchi za kusini mwa Afrika SARPCO yametamatishwa rasmi jijini Dar es salaam.


Katika mashindano hayo timu mbalimbali za majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika zilishiriki huku Zimbabwe ikiibuka mshindi wa mashindano hayo.


Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP,CAMILIUS WAMBURA amesema mashindano hayo yamekuwa na hamasa kubwa si tu kwa michezo bali pia kujenga ushirikiano wa kupambana na uhalifu.


Amesema kupitia mashindano hayo polisi kupitia nchi wanachama sasa watashirikiana kutokeza uhalifu hasa ule uhalifu unaovuka mipaka.


Aidha amesema michezo hiyo itaendelea kuwaunganisha majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika kuongeza tija ya mapambano ya uhalifu unaovuka mipaka kwani kwa pamoja pia wamebadilisha na uzoefu kupitia michezo.

Naye Captain wa timu ya majeshi ya polisi ya Tanzania amesema kuwa michezo hiyo mbali ya kuwajengea uwezo michezoni askari polisi pia imewapa mbinu mbalimbali za kupambana na uhalifu wa aina mbalimbali hasa ule unaovuka mipaka.


Mashindano hayo yalianza septemba mosi mwaka huu na yalishirikisha timu za majeshi ya polisi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Eswatini, Zambia, Msumbiji na wenyeji Tanzania

Comments